Katibu tawala Mkoa wa Mbeya ndugu Rodrick Mpogolo amewataka wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zingine za Mkoa wa Mbeya kwenda kujifunza katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kujua ni kwa namna gani Halmashauri hiyo imefanikiwa kupima maeneo yote ya taasisi ili na wao waweze kufanya hivyo katika maeneo yao kwani kufanya hivyo ni kutekeleza adhima ya serikali ya kuhakikisha maeneo yote ya taasisi yanapimwa .
Kauli hiyo ameisema leo Tarehe 10 Desemba 2024 alipokuwa akikagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Nkung’ungu wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Chunya mnastahili pongezi na niwatake wakurugenzi wengine waje Chunya wajifunze ni kwanini Chunya wameweza kupima maeneo ya tasisi na sasa hivi wako kwenye mchakato wa kuyakatia hatimiliki wakati Halmashauri zingine ukiwauliza swali hili ni mtiani kwao , Afisa elimu utanisaidia kupata takwimu za hali ya upimaji wa taasisi kwenye halmashauri ya wilaya ya chunya na tuwatake wakurugenzi wengine waje wajifunze chunya ,maana hili ni agizo la serikali kuhakiisha maeneo yote ya taasisi za serikali yanapimwa na kuwa na hatimiliki.alisema “.Mpogolo
Aidha Katibu Tawala ametoa siku 14 kuhakikisha miradi wa Ujenzi wa shule Mpya ya Sekondari kata ya Nk’ungu’ngu , Ujenzi wa mabweni 2 na vyumba 6 vya madarasa , ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo Shule ya Msingi Mtande pamoja na ujenzi wa matundu 19 ya vyoo Shule ya Msingi Makongolosi unakamilika huku akiwataka kuongeza rasilimali watu ili kuhakikisha kazi zilizosalia zote zinakamilika
Kaimu Afisa elimu Mkoa wa Mbeya ndugu Robert Mfugale ametoa rai kwa Afisa elimu na wataalamu Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kuhakikisa kazi zilizosalia zinakamilika kwa wakati uliopangwa ili kuwaondolea adha wanafunzi watakoporejea Shuleni kwani serikali imetoa pesa nyingi kwaajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ili kutatua changamoto kwa wananchi.
Afisa Mipango na uratibu Mkoa wa mbeya ndugu Juma Maduhu pamoja na Mkadiriaji wa mejengo QS. Issa Jabiri kwa pamoja wametoa msisitizo kwa wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya pmbali na kukimbizana na muda wanapaswa kuhakikisha taratibu zote za ujenzi zinazingatia viwango vinavyotakiwa pamoja na kuhifadhi nyaraka zote za utekelezaji wa miradi .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona amekiri kuyapokea maaggizo na maelekezo yote yaliyotelewa na Katibu tawala Mkoa wa Mbeya pamoja na wataalamu wake na kuhaidi kuyafanyia kazi kwa wakati uliopangwa kwa kuzingatia Viwango na ubora wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Diwani wa Kata ya Nk’ungu’ungu Mhe Aden Tajak mbali na kumushukuru Mhe. Rais ametoa shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya na Wananchi wa kata hiyo kwa Ushirikiano na usimamizi mkubwa wanaowapa katika kuhakikisha Shule hiyo inakamilika kwani kukamilika kwa Shule hiyo kutawapunguzia adha wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali wa kilometa 12 kwaajili ya kwenda kusoma katika Shule ya Sekondari iliyopo kata ya Lupa.
Katika ziara hiyo ya katibu tawala Mkoa wa Mbeya ametembelea miradi yenye thamani Zaidi ya billion moja na kukagua hatua iliyofikiwa na mambo mengine ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Shule mpya ya sekondari kata ya N’kung’ungu, Ujenzi wa Vyumba vya madarasa na vyoo shule ya Msingi Mtande, Ujenzi wa Mabweni na vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Makongolosi Pamoja na ujenzi wa vyoo Shule ya Msingi Makongolosi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ndugu Rodrick Mpogolo akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Mtande kata ya Mamba Wilayani Chunya.
Kaimu Afisa elimu Mkoa wa Mbeya ndugu Roberth Mfugale akitoa rai juu ya kuzingatia muda wa ukamilishwaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na Matundu ya Vyoo katika miradi mbalimbali ya elimu Wilayani Chunya.
Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Eng Charles Kway akitoa ufafanuzu kwa katibu Tawala wa Mkoa ndugu Rodrick Mpogolo walipotembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari kata ya Nku'ng'ungu Wialayani Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.