Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezitaka Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutenda haki wa wagombea wote watakaowasilisha malalamiko yao kuhusu uteuzi.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akizungumza na Kamati ya Rufaa pamoja na viongozi wa Mkoa wa Manyara katika ziara yake kuangalia maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019.
Amesema tunataka haya malalamiko yanayoendelea huko nje hivi sasa yaishe na kuisha kwake ni ninyi wajumbe wa Kamati hii kufanya kazi yake kwa umakini na uadilifu mkubwa ili kuhakikisha haki inatendeka.
“Tunategemea sana Kamati hizi za Rufaa zilizoundwa katika kila Wilaya Nchini kote, katika kutenda haki na kuweka mambo yote sawa ili kila mtu awe na amani na tukamilishe zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa” alisema Jafo.
Aliongeza kuwa katika mchakato huu msimuonee aibu yeyote na wala msimuonee au kumpendelea mtu katendeni haki kwa watu watakaoleta malalamiko yao kwenu ili kila mtu afurahie Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ukamalike kwa amani
Ndio maana mmechaguliwa kutoka Taasisi za Umma mbalimbali na hamkutoka katika ofisi moja kila mmoja wenu katoka kwenye Taasisi yake hii itasaidia kupunguza mgongano wa maslahi kwa kuwa ninyi wengi hamfanyi kazi katika Serikali za Mitaa.
“Pimeni malalamiko kwa weledi wenu na kufuata Kanuni toeni maamuzi stahiki, Kamati ya Rufaa inaweza ikamrudisha mtu kwenye nafasi yake aliyeenguliwa hapo awali mkiona anastahili kwa mujibu wa vielelezo alivyowaailisha, hii ndio kazi yenu kubwa katika kamati hii” Alisema Jafo.
Aliongeza kuwa wagombea wote ambao kuna baadhi ya vitu wanaona havikwenda sawa huu ndio wakati wa kuviwasilisha kwenu ili muweze kuhakiki na kufanya maamuzi ya busara yanayofuata utaratibu, sheria.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.