kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya ikiongozwa na kaimu katibu Tawala wa Mkoa Ndugu. Donald Bombo imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi itakayo tembelewa, zinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa uhuru September 8, 2022 katika halmashauri ya wilaya ya Chunya
kamati imeridhishwa na miradi iliyochaguliwa na wataalamu na imetaka menejimenti na Uongozi wa halmashauri ya wilaya ya chunya kufanya maboresho madogo madogo ya miundombinu katika miradi itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru ili kusiwepo na dosari katika miradi hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu.Tamim Kambona amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kamati ya Ulinzi na Usalama na kuhaidi kuyafanyia kazi mara moja.
“Yote mliyotuelekeza tutayafanyia kazi na kuhakikisha yanakamilika kwa wakati” alisema Kambona.
Ziara hiyo ya sikumoja imefanyika leo tarehe 01.09.2022 ikiwe zimebaki siku chache Mwenge wa Uhuru kuwasili wilayani humo, ambapo halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwenge wa Uhuru Utatembelea, Utazindua na kuweka Jiwe la Msingi katika miradi Sita {6} ya Maendeleo.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na Zahanati ya Itumba, mradi wa maji Sangambi, Madarasa mawili na Ofisi Mojo shule ya Sekondari Isenyela, Kiwanda cha Kuchakata Dhahabu cha Giant, ujenzi wa daraja la Nselewe na kikundi cha vijana cha Sabasaba group kinacho jishguhulisha na ufyatuaji wa tofali.
Aidha lengo la ziara hiyo kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa sambamba na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ni kujiridhisha na maandalizi yaliyofanya na halmashauri ya Chu nya kwa ajili ya Ujio wa Mwenge wa Uhuru.
PICHA MBALIMBALI WAKATI WA UKAGUZI WA MIRADI YA MWENGE WA UHURU
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.