Mbunge wa jimbo la Lupa wilayani chunya Mhe MASACHE NJERU KASAKA pamoja na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chunya wameridhishwa na ujenzi wa Barabarabara ya Kiwanja Ifumbo inayojengwa kwa kiwango cha Changalawe ili iweze kuruhusu barabara hiyo kupitika kwa Urahisi Zaidi
Mhe.Kasaka kwanza amempongeza mhandisi anayejenga barabara hiyo kwani kazi yake ina matumaini makubwa na ameongeza kuwa kero na adha ya usafiri kwa wananchi waishio kata ya Ifumbo sasa itamalizwa pale ujenzi wa barabara hiyo utakapokamilika tofauti na ilivyokuwa hapo awali usafiri wa Ifumbo ulikuwa ni mgumu sana
“Kwanza nikupongeze Mkurugenzi mtendaji kupitia wahandisi wako kwakupata mkandarasi huyu naona anafanya kazi vizuri na kazi yake ina matumaini kabisa ya kuifungua Ifumbo na hatimaye wananchi wataanza kusafiri kwa urahisi kuja wilayani kupata huduma Mbalimbali” amesema Kasaka
Naye katibu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Cherles Seleman Jokery kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Chunya waliokuwepo katika ziara hiyo amesema lengo la Chama Cha Mapinduzi kupitia ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2023 ni kuhakikisha wananchi wake wanaepukana na kero ya usafiri
“Niwapongeze serikali kwa kuhakikisha mnatekeleza vizuri Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025 hasa kwenye Mradi huu wa ujenzi wa Barabara ya kutoka Kiwanja Mpaka Ifumbo naona mkandarasi anaitendea haki kazi yake
“Sisi kama kamati ya siasa tumerishishwa na maendeleo ya Ujenzi wa barabara kutoka kiwanja mpaka Ifumbo kwani tunashuhudia kwa macho yetu kwamba ujenzi unaendelea vizuri na tunaona Ifumbo sasa inafunguka na hatimaye maisha ya wanaifumbo sasa yatakuwa bora kiuchumi kwani watapeleka bidhaa zao sokoni kwa haraka na kwa urahisi” amesema Jokery
Katika Nyakati tofauti viongozi hao wametoa ushauri kwa ofisi ya Mkurugenzi kupitia mhandisi wa ujenzi wa barabara hiyo kuhakikisha wanaendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili akamilishe kazi hiyo kwa ubora zaidi
Barabara hiyo inajengwa kwa fedha kutoka Mfuko wa Jimbo ambapo Zaidi ya shilingi milioni mia nne zimeshatolewa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ambapo inatarajiwa kukamilika mapema mwezi mei mwaka huu
Kaimu Afisa Mipango wa wilaya Ndugu Godfrey Mwakibinga (Mwenye miwni) kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya akitoa maelezo kwa kamati ya Siasa ya chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya kiwanja - Ifumbo.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.