Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya imemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chunya kumpandisha Cheo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mafyeko kutokana na usimamizi mzuri wa ujenzi wa shule mpya inayojengwa katika kata hiyo.
Hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya Mhe. Dkt Stephene Mwakajumilo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi kukagua utekelezwaji wa miradi ya maendeleo ndani ya wilaya ya chunya ikiwa ni usimamizi wa ilani ya chama cha Mapinduzi.
Dkt. Mwakajumilo aliongeza kusema mradi wa ujenzi wa shule mpya Mafyeko kwa asilimia mia moja hauna shida umesimamiwa na kutekelezwa ipasavyo jambo lililopelekea kamati ya siasa kwa pamoja kukubalinana kwamba Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mafyeko ambaye ndiye msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Shule Mpya kupongezwa.
“Injinia msimamizi wa ule mradi amefanya kazi nzuri sana, mkuu wa shule ndio zaidi tumemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri mara baada ya ule ujenzi wa mradi kuisha yule mkuu wa Shule asiwe mkuu wa shule tena apate nafasi nyingine” alisema Dkt Mwakajumilo
Mweyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Mhe. Dkt Stephene Mwakajumilo pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wameonyesha kutorishwa na utekelezaji na usimamizi wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayoekelezwa ndani ya halmashauri ya wilaya ya Chunya.
“Tumekagua miradi nane ndani ya wilaya ya chunya, tumebaini changamoto baadhi ya maeneo, tuwashauri mkajifunze kwa uongozi wa kata ya mafyeko jinsi ambavyo mnaweza kusimamia vizuri miradi” aisema Mwakajumilo
Ziara ya kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya imedumu kwa siku tatu kuanzia tarehe 21-23/7/2023 na imekagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na mradi wa upanuzi wa Hospitali ya wilaya, mradi wa Mitambo ya kuchimbia visima, Mradi wa Maji Matwiga, Ujenzi wa Shule ya msingi Mafyeko kupitia mradi wa Boost, ujenzi wa nyumba ya watumishi 3 in 1 katika shule ya msingi Sipa, ujenzi wa uzio wa Mnada Sipa pamoja na ujenzi wa barabara Sipa.
Muonekano wa majengo ya Shule mpya ya Msingi Mafyeko
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.