Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imefanya ziara ya siku nne ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Mbugani Mhe. Bosco Mwanginde, imekagua miradi ya elimu na afya lengo ni kujiridhisha na hatua za ujenzi zilizofikiwa ili iweze kutoa huduma bora kwa jamii.
Amesema sekta ya elimu na afya ni sekta muhimu sana na ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya sasa na ya baadaye, hivyo ni vyema kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha miradi hiyo inakamilika na kutekelezwa kwa ubora uliokusudiwa.
Pia aliongeza kwa kusema kukamilika kwa miradi hiyo itasababisha kutoa huduma bora kwa wananchi na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja ujenzi wa kituo cha afya Sangambi, kituo cha afya Kambikaoto, ujenzi kituo cha afya Mafyeko, zahanati ya Itumba, Ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Mtande, pamoja na ujenzi wa soko la madini Mbugani.
Aidha, kamati ilitembelea ujenzi wa shule mpya ya mchepuo wa kiingereza, ujenzi wa jengo la bohari pamoja na wodi ya wanaume na wanawake katika hospitali ya wilaya, ujenzi wa mfumo wa maji katika shule ya msingi Lualaje, ujenzi wa zahanati ya Lyesero , maabara katika shule ya sekondari Mtande pamoja na shule ya sekondari Mtanila.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Hamashauri ya Wilaya ya Chunya, Mhe. Ramadhan Shumbi amesema kuwa ziara zinazofanywa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango zina faida kubwa sana ikiwemo kuchochea kasi ya ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.
“Ziara hizi zinazofanywa na Kamati hii ya Fedha, Uongozi na Mipango, zimekuwa na faida nyingi ikiwemo kuchochea kasi ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kwa sababu kwenye ziara hizo tunaongozana na wataalam wa Halmashauri, hivyo kwenye kila mradi tunapokea taarifa ya utekelezaji.
“Baada ya kupokea taarifa hizo tunaanza kukagua mradi, tukishakagua tunawaambia wataalam mapungufu tuliyoyabaini kisha wataalam wanayafanyia kazi, hali inayopelekea miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa”
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakikagua Ujenzi wa Kituo cha Afya Sangambi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.