Katibu tawala wa wilaya ya Chunya Ndugu Anaklet Michombero amekemea vikali Imani potofu miongoni mwa wafugaji kuhusu chanjo za mifugo jambo linaloweza kudhorotesha ustawi wa mifugo yao, uchumi wa Familia zao, Jamii pamoja na uchumi wa Taifa kwa ujumla
Ametoa wito huo mapema leo 25.08.2025 wakati akizungumza na wafugaji wa kata ya Chalangwa waliojitokeza kwaajili ya zoezi la Chanjo ya mifugo kabla ya kuzindua rasmi chanjo ya mifugo zoezi lililofanyika katika kijiji cha Isewe kilichopo kata ya Chalangwa
“Niwapongeze wafugaji wote kwa kujitokeza kuja kuchanja mifugo. Tunapochanja tunakinga mifugo na magonjwa mbalimbali lakini kwa bahati mbaya watu wanaamini wakichanja mifugo basi mifugo inakufa hii ni dhana potofu na tumeirithi toka vizazi na vizazi naomba tuondokane na dhana hiyo, Lakini pia niwakumbushe kuzingatia maelekezo ya madaktari ili chanjo hii ifanye vizuri na tukifuata taratibu na maelekezo tutashuhudia mabadiriko makubwa katika mifugo wetu” Amesema Michombero
Aidha katibu tawala amewahimiza wafugaji kuwa mabalozi wazuri wa kutoa taarifa kwa Serikali pale wanapoona wafugaji wanahamia Chunya bila kufata taratibu na miongozo na kwakufanya hivyo kutawalinda wafugaji kupata maeneo ya malisho lakini pia kuzuia magonjwa mbalimbalimbali yanaweza kusafirishwa na mifugo waliotoka mkoa mmoja kuingia chunya au kutoka nje ya wilaya
Akitoa taarifa ya zoezi la uzinduzi wa Chanjo hiyo Afisa Mifugo wa wilaya ya Chunya Dkt Benedictor Matogo amesema zoezi la chanjo ya mifugo linataraji kuchanja zaidi ya mifugo laki moja na sabini (170,000) huku Zaidi ya Ngombe laki mbili wanavalishwa heleni kwaajili ya utambuzi wa Mifugo.
Pia dakari Matogo ametoa shukrani kwa Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakutoa vifaa mbalimbali vitakavyotumika kwenye zoezi la Chanjo lakini pia kutoa ruzuku katika zoezi hilo kwani kwakufanya hivyo kumepunguza gharama ya chanjo kwa wafugaji
Zoezi la Chanjo ya Mifugo linataraji kufanyika katika kata zoezi za wilaya ya Chunya na kuwafikia wafugaji katika maeneo wanayoishi huku zaidi ya asilimia tisini na tano ya Kuku tayari wamesha chanjwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Chunya. Chanjo hiyo ikitajwa kusaidia mifugo kukabiliana na magonjwa mbalimbali
Dkt Benedicto Matogo akifafanua jambo Mbele ya Katibu tawala wilaya ya Chunya kabla ya uzidnuzi rasmi wa zoezi la Chanjo ya Mifugo wilaya ya Chunya katika Kijijic cha Isewe kilichopo kata ya Chalangwa
Baadhi ya Ng'ombe wakiwa sehemu lililoandaliwa kwaajili ya Chanjo ya Mifugo tayari kwa Chanjo mapema leo kwenye kijiji cha Isewe kata ya Chalangwa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.