Idara Mtambuka zinazotekeleza shughuli mbalimbali za Lishe zimetakiwa kutengeneza mipango kazi itakayokuwa na shughuli za lishe zenye kuleta matokeo makubwa katika kupambana na kutatua changamoto mbalimbali za masuala ya Lishe ikiwa ni pamoja na udumavu, ukondefu na uzito uliozidi ili kuwa na jamii yenye lishe bora na afya bora .
Kauli hiyo imezungumzwa na Afisa lishe wa Mkoa wa Mbeya bi Josephine Swai leo Novemba 29/224 wakati wa kikao cha maandalizi ya awali ya mipango ya bajeti za Lishe kilichoketi katika Ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Kwenye mipango kazi yetu naomba tujitahidi kupanga shughuli zenye kuleta matokeo makubwa zitakazoenda sambamba na kutatua changamoto mbalimbali katika masuala ya lishe katika jamii ikiwa ni pamoja na masuala ya Udumavu, ukondefu na uzito uliozidi .”amesema Josephine.
Eidha ameongeza kuwa Matarjio ni kuona idara Mtambuka ambazo ni idara ya Maendeleo ya Jamii, Idara ya Kilimo,Idara ya Mipango, Idaya ya Elimu Msingi na Elimu Sekondari katika utekelezaji wa shuguli zake katika masuala ya Lishe unasaidia kupunguza matatizo ya Lishe kwa 80% na asilimia 20% kwa Idara ya Afya
Naye Afisa lishe Wilaya ya Chunya ndugu Saimoni Mayala ametoa rai kwa wajumbe wa kamati ya lishe kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli zinazojumuisha masuala ya lishe katika idara mtambuka ili kuendelea kuifikisha elimu kwa jamii lakini pia kupunguza gharama za utekelezaji kwani elimu zote zitaweza kutolewa kwa pamoja kulingana na shughuli ya Idara husika katika suala la lishe.
Akichangia juu ya suala la changamoto zinazokabili idara mtambuka katika utekelezaji wa shughuli za lishe Dkt Benedicto Matogo amesema kuwa ukomo wa bajeti ndio sababu kubwa ya idara matambuka kutokuwa na shughuli nyingi za lishe kwani katika bajeti hiyo hiyo idara inatakiwa kutekeleza majukumu yake yaliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka husika.
Kikao hicho cha Maandalizi ya awali ya mipango ya Bajeti za lishe kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 kimehudhuriwa na Wajumbe wa kamati ya bajeti ya lishe ya Halmashauri ya Wilaya Chunya, Afisa Lishe Mkoa wa Mbeya na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo suala la kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa jamii kuhusu lishe ile kupunguza na kumaliza kabisa changamoto za ukondefu , udumavu na uzito uliozidi.
Afisa lishe wa Mkoa wa Mbeya bi Josephine Swai akifafanua masuala mbalimbali kuhusu lishe katika kikao cha awali cha mpango wa bejati za lishe kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kilichafanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Afisa lishe Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Saimoni Mayala akizikumbusha idara mtambuka kutengea bajeti shughuli za lishe wakati wa kikao cha maandalizi ya awali ya mpango wa bajeti za lishe
Wajumbe wa kamati ya bajeti ya lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa lishe wa Mkoa wa Mbeya bi Josephine Swai aliye keti mmstari wa mbele katikati baada ya kumaliza kikao cha maandalizi ya awali ya mpango wa bajeti za lishe
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.