Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kwa ujumla kuheshimu mpango wa matumizi bora ya Ardhi akidai ndio njia pekee na sahihi ya kuepusha migororo ya ardhi katika maeneo ya vijiji na kata ndani ya ya wilaya ya Chunya
Ametoa kauli hiyo jana tarehe 6/2/2024 katika mkutano wa Hadhara na wananchi uliofanyika kata ya Lualaje, kijiji cha Lualaje ikiwa ni kawaida yake kuongozana na watalamu kutoka idara na vitendo mbalimbali kwenda kujibu kero za wananchi katika maeneo ya vijiji na kata wanazoishi
“Ndugu wananchi kila kitu kina utaratibu wake, heshimuni mpango wa matumizi bora ya ardhi na watu wa kwanza kabisa kuheshimu mpango wa matumizi bora ya ardhi ni viongozi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya uongozi mpaka ngazi ya juu” alisema Batenga
Aidha Mhe Batenga amewakumbusha wananchi wa wilaya ya Chunya kwamba Mkutano mkuu wa kijiji umepewa uwezo wa kumilikisha ardhi yenye ukubwa wa heka 50 tu, hivyo amewataka kuzingatia hilo ili kuepuka migogoro mbalimbali inayojitokeza ambayo imekuwa kero na inakwamisha maendeleo ya vijiji kwani muda mwingi unatumika kutatua migogoro
“Mkutano Mkuu wa kijiji una uwezo wa kupitisha umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa heka 50 tu na sio vinginevyo, Hatuwezi kuendelea kutengeneza migogoro ya ardhi katika vijiji vyetu, sisi Chunya atakaye kiuka sharia, taratibu na miongozo ya ardhi tutamchukulia hatua kali” alisema Batenga
Diwani wa kata ya Lualaje Mhe Tusalim Mwaijande pamoja na kushukuru miradi mikubwa iliyojengwa katika kata hiyo ambayo ni pamoja na shule ya sekondari Lualaje, Daraja la Lualaje na maeneo mengine mengi amesema kata itawachukulia hatua wazazi wote ambao mpaka sasa hawajawapeleka watoto wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Lualaje.
“Tutawakamata wale wote ambao hawapeleki watoto shule, hatuwezi kujenga miradi kwa gharama kubwa alafu wazazi mshindwe kupeleka watoto shule sisi tutawakamata na kuwachukulia hatua kali” Alisema Mhe Mwaijande
Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi kata ya Lualaje Katibu kata wa Chama hicho ndugu Subira Msindo amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameitendelea haki Ilani ya Chama cha Mapinduzi kata ya Lualaje maana katika kipindi kifupi cha uongozi wake kata imepata Sekondari, Daraja zuri, wahudumu kwenye Zahanati zao, Walimu pamoja na mambo Mengine mengi
Diwani wa kata ya Lualaje Mhe Tusalim Mwaijande akitoa salamu za Kata na kuelezea Miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali ya awami ya sita katika kata ya Lualaje mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya pamoja na wananchi walio udhuria katika mkutano wa Hadhara
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Lualaje walio hudhuria Mkutano wa Hadhari wa Mkuu wa wilaya wenye Lengo la Kusikiliza na kutatua kero zinazo wakabili wananchi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.