Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Chunya imewatahadharisha watumishi wanaoshindwa kusimamia fedha za serikali zinazoletwa wilayani Chunya kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jambo linalopelekea miradi kushindwa kukamilika kwa wakati na wakati mwingine kukosa ubora unaokusudiwa na serikali
Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo nyakati tofauti tofauti mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Bosco S Mwanginde amesema watawawajibisha mara moja watumishi ikibainika kuna matumizi yasiyofuata muongozo wa matumizi ya fedha, utekelezaji wa miradi chini ya kiwango na hata miradi kukosa ubora unaostahili
“Ninyi watumishi na viongozi wa serikali mnaosimamia miradi yetu hakikisheni mnasimamia kwa weledi sisi kama kamati hatuwezi kukubali muharibu fedha za serikali au msimamie hovyo hovyo au mtekeleze mradi chini ya kiwango lazima tutawawajibisha mara moja maana serikali inapoleta fedha huku lengo lake ni kutatua kero za wananchi lakini mkisimamia vibaya maana yake tutashingwa kutatua kero za wananchi” alisema Mwenyekiti wa kamati
Aidha kamati hiyo imetoa maagizo mbalimbali kulingana na mradi husika ambapo baadhi ya maagizo hayo ni kuondoa dawati ambazo hazina viwango ili ziletwe zenye viwango sawa na maelekezo ya serikali, bei ya samani lazima izingatie uhalisia kutoka eneo moja na eneo lingine, lakini pia mafundi ambao hawajakamilisha utekelezaji wa miradi yao wasilipwe mpaka watakapokamilisha kazi zao
Kamati pia imeagiza trekta la Halmashauri ya wilaya pamoja na Lori kupelekwa mara moja kambikatoto ili kupunguza gharama za kubeba mchanga, Kuchota maji pamoja na kubeba mawe ili kuharakisha ujenzi wa shule ya sekondari inayojengwa katika kata hiyo kwani lengo la serikali ni ifikapo Januari mwaka 2024 lazima Shule hiyo ianze
Kamati hiyo ipo kwenye ziara ya Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 Julai-Septemba ambapo miradi yenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia tisa (1,953,104,028) imekaguliwa kwa siku mbili, bado ziara inaendelea siku ya tatu ili kuhitimisha ziara hiyo ambapo kwa siku ya leo tarehe 4/10/2023 kamati itatembelea miradfi yenye thamani ya shilingi milioni mia mbili kumi na mbili (212, 000,000)
Wajumbe wa kamati ye Fedha, Uongozi na Mipango wakiendelea na ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa shule Mpya ya Msingi Kipembawe inayojengwa katika kata ya Mafyeko
Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Mhe Bosco S Mwanginde 9Aliyeshika Fimbo katika na akionekana akizungumza kwa ishara) wakati akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Mhe Bosco Mwanginde (Aliyeshika Ubao kwa mkono wake wa kulia) akikagua namna ubao wa shule ya msingi Kipembawe ulivyowekwa tayari kwa matumizi. Aliyeshika ubao kwa Mkono wa Kushoto ni Diwani wa Kata ya Mafyeko Mhe. Geofrey Z. Kamaka
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.