Katibu tawala wa wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero amezitaka taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na RUWASA wilayani Chunya kulipa mara moja madeni yao huku akisema hakuna malipo yoyote yatakayofanyika kwa taasisi zote ambazo ziko chini ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya mpaka watakapokuwa wamelipa madeni yao kwa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira RUWASA.
Akizungumza leo tarehe 25/05/2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Chunya kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo vyomba vya utoaji maji (CBWSO) vilivyopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya lengo likiwa ni kuhakikisha vyombo hivyo vinajiendesha
“Naomba kutoa maelekezo ambayo Mkuu wa wilaya ameniagiza, Taasisi zote zenye madeni mfano Shule ya Msingi Mapogolo pamoja na Zahanati ya Mapogolo kuhakikisha wanalipa madeni yote, na hili tunaanza sasa hivi kulishughulikia maana taasisi hizo zote ziko chini ya Mkurugenzi hivyo hakuna malipo yoyote yatafanyika mpaka tuone taasisi hizo zimelipa madeni yao kwa RUWASA”. Amesema Michombero
Aidha amewataka viongozi wa Serikali na wadau wengine kutambua mipaka yao ya utendaji kazi jambo ambalo litasaidia kuepusha mwingiliano na migongano ya majukumu kwa viongozi wa Vyombo na viongozi wengine katika eneo husika na kwakufanya hivyo itasaidia vyombo hivyo kuongeza upana wa matumizi ya maji kwa wananchi wa maeneo husika
“Niwaombe sana kila mmoja atambue majukumu yake na wakati mwingine kuheshimu mamlaka moja haikufanyi wewe kuondolewa nafasi yako, Mfano mimi ni mjumbe kwenye kamati mbalimbali na nikiwa katika vikao hivyo natambua muda wa kuwa mjumbe na natambua muda wa kuwa DAS, Hivyo niwaombe viongozi wenzangu kila mmoja atambue mipaka ya majukumu yake” Ameongeza Michombero
Mwakilishi wa meneja wa RUWASA Mkoa wa Mbeya Mhandisi Erasto Vincent Saronga amesema mafanikio makubwa yaliyopo ndani ya RUWASA Chunya yanachagizwa na ushirikiano mzuri uliopo katika ya uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya na uongozi wa RUWASA Chunya, na ameomba ushirkiano huo uendelee ili kwa pamoja waweze kufikia malengo yaliyokusudiwa
Naye kaimu meneja wa RUWASA wilaya ya Chunya Mhandisi Olineno Sanga amesema lengo la RUWASA kuwajengea uwezo viongozi wa vyombo wa watumia maji ni kuhakikisha wanasimamia vizuri makusanyo ya fedha za maji kwenye miradi yao na kuwaongoza katika matumizi bora ya fedha hizo na hatimaye waweze kutatua changamoto za mradi wa maji kwa wakati na kwa uwazi ili wananchi waweze kupata taarifa zote kuhusu miradi ya maji iliyo katika maeneo yao wanayoishi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco Mwanginde amewataka washiriki wote kufuatilia vizuri maelekezo hayo huku akiwahakikishia Madiwani waliopo kwenye maeneo ya miradi ya maji yanayosimamiwa na wananchi kupitia vyombo vya watumia maji kwamba wanapowafuatilia kwa kuhoji maswali lengo lao ni kuona wananchi wanapata maji hivyo wakati mwingine wanaweza kuwauliza viongozi wa vyombo vya watumia maji ili kujiridhisha na mwenendno wa utoaji wa maji kwa wananhi wake.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Tamim Kambona amewataka viongozi wa watumia maji Chunya kuhakikisha wanasimamia vizuri makusanyo ya fedha ili kuweza kuhudumia miundombinu ya maji katika maeneo yao huku akiwataka kutochanganya fedha za maji na fedha nyingine za makusanyo yanayofanyika kwenye vijiji kwani Vyombo vya wasimamia maji ni taasisi inayojisimamia tofauti na taasisi nyingine katika vijiji
Mafunzo hayo yamefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) yakihudhuriwa na Viongozi wa Vyombo kutoka kwenye maeneo husika, madiwani kutoka kwenye maeneo ya miradi husika, watendaji wa kata pamoja na maafisa wa RUWASA kutoka Mbeya na lengo likiwa ni kuwajengea uwezo viongozi hao katika kusimamia miradi ya maji iliyopo katika maeneo yao.
Mwakilishi wa meneja wa RUWASA Mkoa wa Mbeya Mhandisi Erasto Vincent Saronga akisema jambo mbele ya Katibu tawala wilaya ya Chunya wakati wa Mafunzo kwa wajumbe wa vyombo vya watumia maji wilaya ya Chunya
Kaimu meneja wa RUWASA wilaya ya Chunya Mhandisi Olineno Sanga akionesha takwimu za Makusanyo ya Fedha za vyombo vya watumia maji kupitia mfumo (Huko anakoonesha ilikuwa ni eneo ambako projector ilitazamishwa na wataalamu ili kuonesha takwimu kwa mgeni rasmi)
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco Mwanginde akizungumza jambo wakati wa Kikao cha kuwajengea uwezo viongozi wa vyombo vya watumia maji wilaya ya Chunya mapema leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Tamim Kambona akizungumza kwenye kikao cha kuwajengea uwezo viongozi wa watumia maji wilaya ya Chunya kilichoketi mapema leo
Kaimu meneja wa RUWASA wilaya ya Chunya Mhandisi Olineno Sanga akiwasilisha mada wakati wa Kikao cha kuwajengea uwezo viongozi wa vyombo vya watumia maji wilaya ya Chunya
Baadhi ya washiriki wa kikao cha viongozi wa vyombo wa watumia maji wilaya ya Chunya wakiendelea kufuatilia mafunzo na maelekezo kutoka kwa wawezeshaji wakati wa kikao kilichoketi leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.