Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango halmashauri ya wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imeridhishwa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa wilayani humo
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 mwezi Januari – Machi ambapo imekagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi 3 in 1 katika shule za msingi Itete na Sipa, ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika kituo shikizi cha Majiweni, ujenzi wa bweni la Wanafunzi wenye mahitaji maalamu katika shue ya msingi kibaoni, ujenzi wa kituo cha afya mafyeko, ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Mayeka, na ujenzi mradi wa upanuzi wa Hospitali ya wilaya
Akizungumza katika ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amepongeze menejimenti na watendaji kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ya maendeleo ambayo inayotekelezwa kwa fedha za serikali kuu, mapato ya ndani na defha kutoka kwa wadau na wananchi.
Mhe. Mwanginde kwa niaba ya kamati amesema, ni muhimu kwa halmashauri kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa inaleta tija na ina wanufaisha wananchi kwa kiwango kikubwa, hivyo basi ni muhimu kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa iendane na mahitaji ya wananchi na fedha zinazotumika zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Kwa ujumla miradi imetekelezwa kwa kiwango na ubora na thamani ya fedha inaonekana” alisema Mhe, Mwanginde
Aidha kamati imeutaka uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa ndani ya wilaya inakamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi na inakuwa na matokeo chanya katika maendeleo ya hamashauri na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu, Tamim Kambona amepokea pongezi hizo kwa niaba ya watumishi na menejimenti kwa ujumla na ameahidi kuendelea kusimamia na kuhakikisha miradi hiyo inayo tekelezwa ina jengwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati ili kutatua changamoto mbalimbali kwa wananchi.
Ziara ya Ukaguzi wa miradi mbalimbali hufanyika kila baada ya robo ya mwaka wa fedha, na hii ni ziara ya robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikiwa na lengo la kukagua na kushauri mambo mbalimbali ya utekelezwaji wa miradi hiyo ili kuahkikisha thamani ya miradi inaendana na thamani ya fedha zilizotolewa kwa miradi husika.
Wajumbe wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakiendelea na Ukaguzi wa Nyumba ya Watumishi 3/1 katika shule ya Msingi Sipa
Muonekano wa Nyumba ya watumishi 3/1 katika shule ya Msingi Itete kata ya Ifumbo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe, Bosco Mwanginde akieleza jambo wakati wa ziara ya kamati ya Fedha, uongozi na Mipango
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.