Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amewataka madiwani na wataalam kusimamia vizuri fedha zinazotolewa kwaajili ya utekerezaji wa miradi katika maeneo yao ili miradi hiyo iweze kuwa na tija na kuendana na thamani ya fedha kwani kwenye ukusanyaji wa mapato Halmashauri inafanya vizuri na kutaka fedha hizo zipelekwe kwenye utekelezaji wa miradi kwa maslahi ya wanachunya na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ameitoa leo 25 Aprili 2024 wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa robo ya Tatu uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Pamoja na kufanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato basi lengo iwe ni kupeleka fedha hizo kwenye miradi yetu, niombe kila mtaalam ambaye mradi unatekelezwa katika kata au kijiji basi aweze kusimamia fedha hizo vizuri na kuhakikisha mradi unakamilika, lakini pia niwaombe waheshimiwa madiwani, fedha hizi tunazozisema kwamba zimekusanywa zinakwenda kutekeleza miradi huko kwenye maeneo yetu basi tukazisimamie ili wananchi wetu wanufaike”amesema Mhe.Mwanginde
Aidha Mhe. Mwanginde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa ukusanyaji mzuri wa mapato na kuvuka lengo lililokusudiwa kwa kukusanya asilimia 142 mpaka tarehe 5 April 2024.
Akizungumza katika Mkutano wa baraza la Madiwani Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbarak Alhaji Batenga ameelezea mpango mkakati wa Kuanzisha Kongani za malisho katika tarafa ya kiwanja na kipembawe za halmashauri ya Wilaya ya Chunya mpango ambao utasaidia kutatua changomoto mbalimbali za wafugaji hususani katika suala zima la malisho pamoja na kupunguza migogoro baina ya wakulima , wafugaji na wachimbaji.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Charles Seleman ametoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ,Baraza la Madiwani na Watumishi kwa utekelezaji mzuri wa Shuguhuli za maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya pamoja na utatuzi wa kero za wananchi na kuwataka weendelee kutatua kero mbalimbali za wananchi katika maeneo yao kwaajili ya kuwaletea maendeleo Wanachunya na Taifa kwa ujumla.
Akitoa shukrani kwa niaba ya madiwani Mhe. Tusalim Mwaijande Diwani wa kata ya Lualaje amekiri kuwa wamepokea maelekezo yote kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kwaajili ya Utekelezaji sambamba na hilo amedhauri Madiwani kuendelea kuwaelimisha viongozi wa kata na vijiji katika maeneo ambayo kongani za malisho zitajengwa .
Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya tatu kimeketi leo katika Ukumbu wa MikutRT0ano Jengo Jipya la Utawala na kimehudhuriwa na Madiwani, Mkuu wa Wilaya , Katibu wa Chama cha Mapinduzi ,Wakuu wa vitengo katika halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Wadauu kutoka taasisi mbalimbali,Vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amewataka madiwani na wataalam kusimamia vizuri fedha zinazotolewa kwaajili ya utekerezaji wa miradi katika maeneo yao ili miradi hiyo iweze kuwa na tija na pendant na thamani ya fedha kwani kwenye ukusanyaji wa mapato Halmashauri inafanya vizuri na kutaka fedha hizo zipelekwe kwenye utekelezaji wa miradi kwa maslahi ya wanachunya na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ameitoa leo 25 Aprili 2024 wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa robo ya Tatu uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Pamoja na kufanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato basi lengo iwe ni kupeleka fedha hizo kwenye miradi yetu, niombe kila mtaalam ambaye mradi unatekelezwa katika kata au kijiji basi aweze kusimamia fedha hizo vizuri na kuhakikisha mradi unakamilika, lakini pia niwaombe waheshimiwa madiwani, fedha hizi tunazozisema kwamba zimekusanywa zinakwenda kutekeleza miradi huko kwenye maeneo yetu basi tukazisimamie ili wananchi wetu wanufaike”amesema Mhe.Mwanginde
Aidha Mhe. Mwanginde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa ukusanyaji mzuri wa mapato na kuvuka lengo lililokusudiwa kwa kukusanya asilimia 142 mpaka tarehe 5 April 2024.
Akizungumza katika Mkutano wa baraza la Madiwani Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbarak Alhaji Batenga ameelezea mpango mkakati wa Kuanzisha Kongani za malisho katika tarafa ya kiwanja na kipembawe za halmashauri ya Wilaya ya Chunya mpango ambao utasaidia kutatua changomoto mbalimbali za wafugaji hususani katika suala zima la malisho pamoja na kupunguza migogoro baina ya wakulima , wafugaji na wachimbaji.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Charles Seleman ametoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ,Baraza la Madiwani na Watumishi kwa utekelezaji mzuri wa Shuguhuli za maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya pamoja na utatuzi wa kero za wananchi na kuwataka weendelee kutatua kero mbalimbali za wananchi katika maeneo yao kwaajili ya kuwaletea maendeleo Wanachunya na Taifa kwa ujumla.
“Niwaombe waheshimiwa madiwani na watalaam mbalimbali tusizifuge kero za wananchi bali tukazitatue kero za wananchi tumeagizwa kila diwani apange walau siku moja kwa wiki kusikiliza na kutatua kero za wananchi”alisema Seleman
Akitoa shukrani kwa niaba ya madiwani Mhe. Tusalim Mwaijande Diwani wa kata ya Lualaje amekiri kuwa wamepokea maelekezo yote kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kwaajili ya Utekelezaji sambamba na hilo amedhauri Madiwani kuendelea kuwaelimisha viongozi wa kata na vijiji katika maeneo ambayo kongani za malisho zitajengwa .
Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya tatu kimeketi leo katika Ukumbu wa MikutRT0ano Jengo Jipya la Utawala na kimehudhuriwa na Madiwani, Mkuu wa Wilaya , Katibu wa Chama cha Mapinduzi ,Wakuu wa vitengo katika halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Wadauu kutoka taasisi mbalimbali,Vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Alhaji Batenga akielezea mpango wa kuanzisha kongani za malisho katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwenye Mkutano wa baraza la Madiwani robo ya tatu uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) ndugu Charles seleman akitoa salam za Chama kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya tatu uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Diwani wa kata ya Lualaje Mhe. Tusalim Mwaijande akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waheshimiwa Madiwani kabla ya kuhailishwa kwa Mkutano wa baraza la madiwani robo ya tatu uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri .
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.