Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imewataka wanawake, vijana na wale wenye ulemavu walionufaika na mkopo wa asilimia 10 ambazo ni fedha za serikali zinazotokana na mapato ya Ndani kuhakikisha matunda ya kukopeshwa kwao yanaonekana kwa walengwa kwanza na baadaye kwa jamii inayowazunguka kwakufanya hivyo mtakuwa mmetiza lengo la serikali la kuwainua wananchi wake kiuchumi
Hayo yametolewa mwishoni mwa juma wakati kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ilipotembelea kikundi cha Wanawake Jamii kilichopo kata ya Lupa ili kujionea shughuli zinazofanywa na kikundi hicho tangu kilipoanza kukopeshwa na Halmashauri ya wilaya ya Chunya mwaka 2019 kwa fedha zinazotengwa kwaajili ya kuwakopesha vijana wanawake na wenye ulemavu maarufu kama asilimia kumi
“Kile mnachokipata kama faida lazima tukione kwenu kama wanakikundi na baadaye tukione kwa jamii inayowazunguka, nje ya hapo maana ya lengo la ninyi wanawake, vijana na wenye ulemavu la kukopeshwa na Serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan litakuwa bado halijatimia hivyo lazima tuone mabadiliko kwanza kwenu ninyi wenye na baadaye jamii yenu” Amesema Mhe Shumbi
Kamati hiyo pia imewapongeza wanawake wa kikundi hicho kwakurejesha fedha walizokopeshwa lakini pia kwa namna ambavyo hawakukata tamaa baada ya mradi wa kufuga kuku kushindwa kuendelea kutokana na changamoto mbalimbali na kuamua kuhamia kwenye mradi wa kufuga Nyuki huku lengo lao likibaki kuwa la kujikwamua kiuchumi
Kamati hiyo imewashauri kikundi cha wanawake Jamii kuona uwezekano wa kumiliki misitu yao wenyewe ili kurahisisha utekelezaji wa mradi wao wa ufugaji wa Nyuki jambo litakalo wasaidia kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu kwenye misitu mbalimbali ambayo ndiyo hutumika kama maeneo yao ya kuweka mizinga
Wakati akitoa taarifa ya miradi wa kikundi hicho mwenyekiti wa kikundi Bi Vumilia Kilindu amesema faida wanazopata wanakumbuka kurudisha kwa jamii inayowazunguka kwani mpaka sasa wamechangia mifuko kumi ya saruji katika ujenzi wa shule ya Msingi Lupatingatinga, wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya laki tano (500,000) kwa wanafunzi wasiojiweza kwenye shule ya msingi Lupatingatinga na wataendeleo kufanya hivyo
Akitoa salamu za Shukrani kwa kamati hiyo Mhasibu wa kikundi hicho Bi Delista Hyera ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwanza kuwakopesha fedha na kuendelea kuwapa ushauri wa mara kwa mara, pamoja na kutembelewa na maafisa maendeleo ya Jamii lakini amesema ushauri na maelekezo ya kamati hiyo wameupokea kwa dhati na wataufanyia kazi ili waendelee kufanya vizuri zaidi
Kikundi hicho mpaka sasa kina jumal ya wanachama 16, kina miliki mzinga Zaidi ya mia mbili ambapo 151 tayari imewekwa katika msitu mbalimbali na 57 iko tayari muda si mrefu itapelekwa kwenye msitu wa Inyonga ulioko kata ya Mafyeko na huwa wavuna karibu lita mia tano za asali na kuziuza hatimaye kuboresha maisha yao kama wanakikundi na baadaye kurudisha kwa jamii inayowazunguka
Mjumbe wa kamati ya Fedha Uchumi na Mipango Mh. Benson B. Msomba Diwani wa Kata ya Kasanga akichangia jambo mbele ya wana Kikundi cha ufugaji wa Nyuki kilicho Lupa
Mh. Phide K. Mwalukasa mjumbe wa kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango Halmashauri ya wilaya ya Chunya akichangia jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea kikundi cha wanawake jiamini kilichopo Lupa
Bi Vumilia Kilindu Mwenyekiti wa miradi wa kikundi cha wanawake Jiamini akisoma taarifa ya kikundi mbele ya Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya pindi walipotembelea kuona maendeleo ya kikundi hicho
Bi Delista Hyera ambaye ni Mhasibu wa kikundi cha Mwanamke Jiamini kilichopo Lupa akitoa shukrani zake kwa kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango walipotembelea kukagua maendeleo ya kikundi hicho ambapo ni wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.