Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona amezipongeza timu za Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa uwakilishi mzuri katika mashindano yaliyoandaliwa na shirikisho la michezo Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Ametoa pongezi hizo leo tarehe 02 November, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya uliopo jengo jipya la utawala wakati akikabidhiwa vikombe pamoja na medali za ushindi kutoka kwa timu za Halmashauri ya Chunya zilizoshiriki Michezo Mbalimbali SHIMISEMITA iliyotamatika hivi karibuni Jijini Dodoma.
“Niwapongeze wote ambao mmekwenda Dodoma kwenye mashindano haya mmeshiriki na matokeo yake tumeyaona niwapongezeni sana kwa hilo na sasa Tujipange kwa Mwaka unaokuja tufanye maandalizi ya kutosha ili tukafanye vizuri zaidi, tumesha anza kutengeneza uwanja wetu wa mpira pale (Mbugani) na lengo tuwe na uwanja waFootball, Netball, Volleyball pamoja na Basketball yaani tuwe na viwanja vyote” alisema Kambona
Pia Kambona amemwagiza Mkuu wa Idara ya Utumishi Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha Idara na vitengo vyote vinatenga bajeti za michezo kwa mwaka 2024/2025 ili kuhakikisha timu yetu inashiriki michezo yote kwa mashindano ya SHIMISEMITA mwaka 2024
“Afisa Utumishi kwenye bajeti ya Mwaka ujao tukubaliane sasa kila idara zitenge fedha za michezo ili kurahisisha ushiriki wa timu yetu kwa kipindi kijacho au tukiona inafaa tupunguze bajeti za idara na vitengo ili fedha zote za michezo zikae kwa Mkurugenzi kwa maana ya utawala ili muda ukifika tunakuwa na uhakika wa bajeti”.
Awali akitoa taarifa ya safari iliyodumu kwa siku 14 kiongozi wa msafara huo ambaye pia ni mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu Vicent Msolla pamoja na kumshukuru Mkurugenzi mtendaji kwa namna alivyowawezesha kushiriki mashindano hayo ameomba kuendeleza mazoezi pamoja na kupata Makocha wenye weledi wa kuwaongoza katika mazoezi hayo jambo litakaloleta mafanikio makubwa zaidi mwaka ujao.
Timu za halmashauri ya wilaya ya chunya zimeshiriki michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa pete wanawake, mpira wa Mikono Handball kwa Wanaume na wanawake, Mchezo wa Kuvuta kamba wanaume na wanawake, Kurusha Tufe wanaume na wanawake, Riadha, Karata pamoja na Mchezo wa Bao..
Halmashuri ya wilaya ya Chunya katika mashindano ya SHIMISEMITA 2023 imefanikiwa kutwa makombe mawili (2) na Medali Moja (1) Kuvuta kamba Wanaume Mshindi wa kwanza, Kuvuta kamba Wanawake Mshindi wa Tatu na kurusha Tufe Mshindi wa Tatu kwa Upande wa Wanaume
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona (kulia) akikabidhiwa Cheti cha Ushiriki wa SHIMISEMITA 2023 na Kiongozi wa Msafara Ndugu Vicent Msolla
Ridhawani Mshighati Kepteni wa timu ya wanaume kuvuta kamba na mwakilishi wa timu ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Kurusha Tufe akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji Medali ya ushindi wa Tatu kurusha Tufe
Kepteni Msaidizi wa timu ya wanawake kuvuta kamba Bi Joyce Kisula akimkabidhi kombe la mshindi wa tatu kwa timu ya Halamshauri ya wilaya ya Chunya Kuvuta kamba (KE) Mkurugenzi Mtnedaji wilaya ya Chunya
Mkurugenzi mtednaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona akipeana mkono na Ndugu Vicent Msola Kiongozi wa Msafara wa timu ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati wa Hafla ya kukabidhi makombe na medali mapema leo
Mkurugenzi mtednaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona (Aliyeshika Makombe) akifurahia ushindi wa timu za Halmashauri katika Mashindano ya SHIMISEMITA 2023 yaliyotamatika Jijini Dodoma (Kushoto kwa Mkurugenzi ni Afisa utumishi na Utawala Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu John Mahalani
Afisa utumishi na Utawala wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu John Maholani (Aliyeshika cheti na Kombe katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Timu iliyoshiriki mashindano ya SHIMISEMITA 2023 jijini Dodoma
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.