Mkuu wa wilaya ya chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka amewataka watendaji ngazi ya Halmashauri, kata na vijiji kuhakikisha wanaweka mikakati itakayopolekea kuendelea kushika nafasi ya tatu au nafasi ya kwanza katika kutekeleza afua za lishe ili kuwa na jamii yenye afya bora kwa ustawi wa Chunya na taifa kwa ujuma
Ameyasema hayo December 4, 2023 katika kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa halmashauri (Jengo jipya), chenye lengo la kupokea na kupitia utekelezaji wa tathimini ya hali ya lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Mhe Mayeka amewataka watendaji ngazi zote kuweka mikakati zaidi na kuhakikisha nafasi waliyopata haishuki bali waendelee mbele Zaidi kuhakikisa wanapata nafasi ya pili na nafasi ya kwanza
“Naamini kwa spiriti mliyo nayo na kwakuwa tumeshaonja kuwa kwenye nafasi hizi sitarajii kama tunaweza tukatoka zaidi ya kuendelea mbele zaidi” alisema Mhe. Mayeka
Mayeka amewataka Watendaji wa kata kuyatekeleza yale yote yanayoamuliwa katika vikao ili kuhakikisha utekelezaji wa mkataba wa lishe unafanyika kwa nguvu na kwa hari kubwa ili wasipoteze nafasi waliyopo
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Tamim Kambona amesema lengo la Halmashauri ni kutoka nafasi ya tatu waliyoishika kwa miaka miwili mfululizo na kushika nafasi ya kwanza kwa mwaka Ujao
“Tumekuwa wa tatu mwaka jana na tumekuwa wa tatu mwaka huu hatutaki tena nafasi ya tatu tunaitaka namba moja au namba mbili lakini lengo la kwangu mimi ni namba moja” alisema Kambona
Kambona amesema kuwa kwa vigezo vilivyopo katika utekelezaji wa afua za lishe wanao uwezo wa kushika nafasi ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024, aidha ameongeza kua kwa bajeti inayokuja Halmashauri itanunua gari kwaajili ya kutekeleza shughuli za lishe.
“Bajeti ya mwaka huu tunayokwenda kuiandaa mweka hazina upo na afisa mipango upo tunataka tununue gari ya lishe” alisema kambona
Kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya , Katibu tawala ,badhi ya Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri, Maafisa lishe ngazi ya Wilaya na Kata pamoja na watendaji wa Kata katika wilaya ya Chunya.
Wajumbe wa kikao cha tathimini ya lishe wakifwatilia agenda zinazoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Darson Andrew akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S.Mayeka kama kinara wa Lishe
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.