Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S.Mayeka amewataka wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) kuwa mfano wa kuigwa kutokana na mambo mbalimbali ambayo wamejifunza yatakayo wawezesha kuisaidia jamii na Taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja ulinzi na usalama, kuwa tayari watakapohitajika katika mambo mbalimbali ya kujenga Taifa .
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 11/11/2023 wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) katika viwanja vya mpira wa miguu Bitimanyanga katika kata ya Mafyeko yaliyohudhuriwa na washiriki zaidi ya mia moja na sabini (170) na yamedumu zaidi ya siku tisini (90)
“Mkawe mfano wa kuigwa katika jamii kwa kufanya mambo mazuri ya kuisaidia jamii na kuwa tayari kutekeleza majukum yenu mliyofundishwa pale mtakapohitajika katika mambo mbalimbali yanayoweza kujitokeza kama vile uharibifu wa mazingira, mafuriko, ajali na majanga mengineyanayoweza kutokea katika vijiji vyenu na Taifa kwa ujumla” amesema Mh. Mayeka.
Aidha Mhe. Mayeka amewataka wananchi kuheshimu mafunzo hayo yanapojitokeza kwa awamu nyingine na kuacha kubeza kwa kutoa maneno yasiofaa kuipotosha jamii kuhusu mafunzo hayo kwani mafunzo ya Mgambo yapo kwa mujibu wa sheria hivyo watakaoonekana kubeza mafunzo hayo hatua zitachukuliwa zidi yao.
‘’Wananchi mafunzo ya Mgambo ni kwa mujibu wa sheria hata Mhe. Rais anajua Mafunzo haya lakini kuna wananchi hawajui kama kubeza au kutoa maneno yasiyofaa juu ya mafunzo haya ni kinyume na sheria, niombe sana yatakaporudi mafunzo haya kwa kipindi kingine wananchi mjitokeze kwa wingi na wale wanaobeza na kuongea maneno yasiyofaa waache na wajue ni kinyume cha sheria wanaweza wakachukuliwa hatua alisema Mhe. Mayeka”
Naye mwakilishi wa Mshauri wa mafunzo ya Mgambo wa Mkoa Luteni Ngaji Vinac Ipela amewataka wahitimu wa mafunzo ya Mgambo kwendelea kuwa wazalendo na wakakamavu na wenye utayari wa kuisadia jamii na Taifa pale watakapohitajika kutekeleza majukum yao kwani Taifa linawategemea.
Akisoma risala kwa Mgeni rasmi mmoja ya wahitimu wa mafunzo ya Mgambo ndugu Ramadhani Kasambandege amesema kuwa katika kipindi chote cha mafunzo wameweza kujifunza mambo mbalimbali kwa nazalia na vitendo ambayo yatawasaidia wao kama viajana kuweza kujipatia ajira lakini pia kuisaidia jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla .
“ Kwakipindi chote cha mafunzo tumejifunza mambo mbalimbali kama vile ujasiriamali, mbinu za kivita, huduma ya kwanza , zimamoto na uokoaji, kwata , usomaji wa ramani, utimamu wa mwili, usalama wa raia, kuzuia na kupambana na rushwa, kuzuia wahamiaji haramu na mengine mengi” alisema Ramadhani.
Awali akitoa salamu zake diwani wa kata ya Mafyeko Mhe.Jofre Kamaka Amewapongeza vijana waliofanikiwa kuhitimu mafunzo ya mgambo na kuwataka wakayafanyie kazi yale yote waliyojifunza na kuibadilisha jamii kwa mambo mazuri ikiwa ni pamoja kuonyesha uzalendo kwa nchi yao na kuisaidia jamii pale inapowahitaji..
Mafunzo ya mgambo yalianza 3/7/2023 na kuhitimishwa leo 11/11/2023 ambapo jumla ya vijana 177 kutoka katika kijiji cha Bitimanyanga na Mafyeko ambapo wanaume 144 na wanawake 30 wamehitimu Mafunzo hayo ambapo masomo mbalimbali yamewasilishwa kwa washiriki wa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na Changamoto zozote zinazoweza kujitokeza katika jamii na Taifa kwa ujumla wake
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka akisalimiana na viongozi waliojitokeza kumpokea wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya Jeshi l akiba (Mgambo) leo katika viwanja vya mpira wa Miguu Bitimanyanga
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S ,ayeka akikagua vijana wahitimu wa mafunzo ya jesho la Akiba (Mgambo) katika viwanja vya Mpira wa miguu Bitimanyanga
Askari wa jeshi la akiba (Mgambo) wakitoa salamu kwa Mgeni rasmi wakati wa Hafla za ufungaji wa Mafunzo ya Jeshi hilo katika viwanja vya mpira wa Miguu Bitimanyanga
Askari wa jeshi la akiba (Mgambo) pamoja na wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya jeshi la akiba Bitimanyanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chunya akitoa hotuba katika Hafla hiyo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.