Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka amewaasa wananchi wa wilaya ya Chunya kuzingatia suala la usafi katika maeneo yao huku wakijua Chunya ni ya wananchi wenyewe na amewaagiza viongozi wa kata kutumia sheria ndogo za Halmashauri ili kuwachukulia hatua wale watu wanaokiuka suala la usafi katika mazingira yao kwani waweza kusababisha magonjwa ukizingatia msimu tunaouendea ni msimu wa Mvua
Ametoa wito huo mwishoni mwa juma wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ifumbo katika Mkutano wa hadhara baada ya kukamilika kwa ziara ya kamati ya usalama wilaya pamoja na wataalamu mbalimbali kukagua shamba lenge mgogoro kwa watu wa familia moja na kulipatia ufumbuzi sauala hilo
“Suala la usafi mlisimamie. Sheria ndogo ndogo za Halmashaurin zipo zinazoeleza adhabu mbalimbali kwa watu wanaokiuka taratibu zetu, zitumieni, msisubiri msukumwe. Sasa hivi tunaenda kwenye msimu wa Mvua tutapata kipindupindu na nyiniyi mnakumbuka hapa tumehangaika na kichocho, sasa ili tusiendelee kuhangaika na Magonjwa haya tena tafadhari zingatieni suala la usafi na mimi niwaombe kila mtu ajisimamie mweyewe kwenye kaya yake maana mji huu ni wa kwenu. Mimi natoa maagizo mtendaji wa kata mtendaji wa kijiji wapeni siku saba kila mtu afanye usafi kwenye maeneo yake na yeyote atakaye kiuka kamateni waleteni Chunya ili sheria ichukue mkondo wake
Awali akitoa salamu za wananchi wa kata ya Ifumbo kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya Diwani wa kata hiyo Mh. Weston S. Mpyila ameishukuru serikali kwa ujumla wake kwa namna inavyowajali wananchi wa ifumbo kwa kuendelea kutoa fedha ili kujenga miradi mbalimbali yenye manufaa kwa wananchi ikiwepo sekta ya Afya, Sekta ya Barabara, sekta ya Elimu, sekta ya Maji na maeneo mengine
“Sasa hivi tuna zahanati Luparmeket na imekamilika na inatoa huduma, wananchi wanawapongeza sana serikali kwa ujenzi huo Mhe Dc kitua cha afya kimeanza kujengwa toka 2016 lakini bado hakijakamilika, Milioni 77 zinahitajika kukamilika Lakini na wewe mhe Dc unaweza kulisemea jambo hilo ili kituo hicho kiweze kukamilika lakini pia Tukupongeze sana kwenye eneo la miundombinu wananchi wanashukuru kwa ujenzi wa barabara ya Kiwanja mpaka hapa ifumbo lakini tunaomba eneo la kilometa 1 lililobakia basi Mungu akiwajalia pia palekebishwe”
Ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Chunya ilihusisha wataalamu toka sekta ya madini ambapo Ndugu Laurent Mayalla ambaye ni afisa madini Mkazi wilaya ya Chunya amewaahidi wananchi wa kata ya Ifumbo kufika katani hapo kutoa elimu ya Madini ili wananchi wengi zaidi nao washiriki kwenye mchakato wa uchimbaji na uchakataji wa madini
Nashukuru kwa fursa hii madini ni maisha na utajiri, Serikali ya awamu ya sita inatawaka wananchi mshiriki kwenye sekta hiyo na nimemsikia Mhe Diwani kwamba kuna wananchi wanataka kushiriki huko hivyo niwaahidi jumatano kwenye ofisi ya kata wenye kutaka kushiriki kwenye mambo ya madini tukutane pale tujadiliane ili tuoine namna gani mtashiriki ipasavyo.
Diwani wa kata ya Ifumbo Mh. Weston S. Mpyila akitoa salamu za wananchi wa Ifumbo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati wa mkutano wa Hadhara na wananchi wake
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa Hadhara wakiwa tayari kumsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chunya alipofika Ifumbo kuzungumza na wananchi wa Ifumbo
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka aliyenyoosha mkono akioneshwa mipaka ya Shamba lenye mgogoro balipofanya ziara katika kata ya Ifumbo ili kutatua mgogoro huo
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S. Mayeka (Mwenye shati la Blue na yuko katika aliyeinua mkono) akizungumza na wananchi wenye mgogoro wa Shamba ambao ni kaka na Mdogo wake wa kike
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.