Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka Saimon Mayeka amewataka wananchi na Viongozi kutokubeza mafunzo yanayotolewa kwa Mgambo kwani mafunzo hayo yanawajenga vijana kuwa wazalendo kwa nchi yao Lakini pia watasaidia katika shughuli mbalimbali za maendelao na ulinzi kwa jamii yao na Taifa kwa Ujumla
Kauli hiyo ameitoa 28/07/2023 wakati akifungua rasmi mafunzo ya Mgambo yanayofanyika kijiji cha Bitimanyanga kata ya Mafyeko ambapo vijana kutoka katika vijiji viwili (2) kijiji cha Mafyeko na Kijiji cha Bitimanyanga ambapo jumla ya vijana 387 wamejitokeza katika mafunzo hayo 387 wanaume wakiwa 345 na wanawake 42
“Kubeza na kutoa kauli zisizo faa kuhusiana na mafunzo ya Mgambo ni kosa na wote watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua, Viongozi mpo hapa mnanisikia yeyote atakayetoa maneno ya siyofaa na kubeza Mafunzo haya akamatwe kwasababu mafunzo haya yapo kwa mujibu wa Sheria na yanafanyika Nchi nzima na yanafanyika kwa kalenda inayofanana, na ninyi vijana mliojitokeza kushiriki mafunzo ya Mgambo mmefanya uamuzi sahihi.’’ Alisema mhe Mayeka
Pia amewataka vijana wote wanaopata mafunzo ya Mgambo kuwa makini na mafunzo wanayoyapata na kuhakikisha wanafuatilia kila hatua na kuelewa vizuri pia kupokea maelekezo yote yanayotolewa na wakufunzi kwa vitendo kwani watajifunza mambo mengi mazuri yanayoendana na mabadiriko ya kidunia.
‘’Niwatake vijana wote mnaoshiriki mafunzo haya kuwa makini na kufuatilia kwa vitendo, msifanye mafuzo haya kwa ulegevu na uzembe kama umekuja kupoteza muda unapaswa kubadilika, ulivoingia uwe tofauti na utakavyo toka kwani mtajifunza mambo mbalimbali kama masuala ya Rushwa, Usalama wa Nchi , mazingira ,matumizi ya silaha na mambo mengine mengi ili mtakapomaliza mkafanye majukumu yenu kwa ukamilifu”
Akitoa salam katika ufunguzi wa mafunzo hayo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco Said Mwanginde amewataka vijana wote wanaopata mafunzo hayo kutambua kwamba wao ni wanajeshi hivyo wanapaswa kuwa wazalendo katika jamii na nchi kwa ujumla kwani jamii itawategemea sana kwa masuala ya ulinzi katika Jamii na katika kulijenga Taifa.
‘’Ninyi vijana lazima muwe wazalendo na Nchi yenu lazima mtambue mmeingia kwenye mfumo wa kuwa walinzi hivyo jamii itawategemea sana katika masuala ya ulinzi kwahiyo mjifunze mafunzo haya kwa manufaa yenu wenyewe na Taifa lenu na mtakapo fuzu mafunzo haya tunataka kuona jamii , kijiji na wilaya inanufaika na ninyi kupitia mafunzo mliyoyapata” alisema Mhe Mwanginde.
Awali akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi Mkufunzi na mshauri wa Mgambo wilaya ya Chunya Captain Mohamed Ali Omary amesema changamoto inayokabili mafunzo hayo ni baadhi ya wananchi na Viongozi kubeza mafunzo hayo na kuwashawishi baadhi ya vijana kuacha mafunzo hayo na kusababisha baadhi ya vijana kuacha mafunnzo hayo hali inayopelekea kupungua kwa idadi ya wanafunzi .
Ufunguzi wa mafunzo hayo rasmi wa Mafunzo hayo umefanyika tarehe 28/7/2023 Na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa kata na vijiji, Viongozi wa chama cha Mapinduzi pamoja na Kamati ya Usalama na mafunzo hayo yalianza rasmi tarehe 3/7/2023 yanarataji kudumu kwa miezi minne (4) na hufanyika kila mwaka pia ni zoezi la Nchi nzima
Baadhi ya vijana waliojitokeza katika mafunzo ya Mgambo mwaka huu wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo haya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.