MKUU wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka Simon Mayeka amewaagiza wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari kuhakikisha walimu walioko masomoni wanatengewa vishikwambi vyao ili watakaporejea pasitokee upungufu wowote wa vitendea kazi kwani Serikali imepanga kuwapatia vitendea kazi hivyo walimu wote
Akikabidhi vishikwambi 324 kwa walimu mapema leo ofisini kwake amewataka kuendelea kuvitunza vitendea kazi hivyo huku akisisitiza kutumiwa na watu waliokusudiwa
Mayeka amewaagiza maafisa elimu wilaya kuhakikisha wanavitunza vishikwambi vya walimu waliopo masomoni na kukabidhiwa pindi watakapo rejea kutoka masomoni
“Afisa Elimu vifaa vyao wale ambao wapo masomoni baada ya kumaliza masomo wapewe vitendea kazi hivyo, sitarajii kuona vinatumika kwa mtu ambaye siyo muhusika kwa maana asiye mwalimu” amesema Mayeka
Kwa niaba ya walimu waliokuwa wamekosa vitendea kazi hivyo wakati wa ugawaji wa awali, wameeleza furaha yao na kuishukuru serikali kuwajali na kuwarahisishia utendaji kazi wao bila kujali jinsi, elimu, nafasi au eneo analofanyia kazi mwalimu
“Sisi kama walimu tunaweza kupata vitabu vyovyote mtandaoni, kwa jitihada hii iliyofanywa na serikali inaturahisishia sana sisi walimu katika utendaji kazi wetu na tuna ahidi tutavitumia kama ambavyo serikali imekusudia” amesema Mwalimu Omary Mkalimoto
Ikumbukwe mapema mwanzo mwa mwezi Januari Mkuu wa wilaya hiyo aliongoza zoezi la ugawaji wa vishikwambi kwa walimu ambapo vishikwambi 594 viligawiwa na leo amehitimisha zoezi hilo kwa kugawa vishikwambi 324 na kufikisha jumla ya vishikwambi 918 kama idadi ya walimu wote wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka wakwanza kutoka kulia akimkabidhi kishikwambi Mwalimu Omary Mkalimoto kutoka Shule ya Sekondari Kiwanja
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.