Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka amewataka wazazi na walezi wa watoto wilayani Chunya kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja ili kuwapatia watoto lishe bora itakayowasaidia kukua vizuri na hata kuwa na uwezo mzuri wa akili darasani jambo litakalosaidia kupata Taifa lenye watu imara hapo Mbeleni
Mhe Mayeka ametoa Kauli hiyo jana Julai 4, 2023 ambapo alikuwa Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya lishe na Afya ya kijiji ambayo huadhinishwa kila roba ya mwaka ambapo jana maadhimisho hayo yamefanyika kiwilaya katika kijiji cha Isangawana kilichopo kata ya Isangawana
“Ukizembea kwenye Mambo ya Lishe lazima uone tofauti ya Makuzi kati ya Mtoto wako na mtoto wa jirani yako na wala usianze kutafuta mchawi, ni uzembe wenu baba na Mama wa mtoto maana MUNGU amegawa vyakula vya makundi yote katika kila eneo, hivyo kukosa lishe bora kwa mtoto wako ni suala la uzembe tu na kupuuzia mnapopewa Elimu na wataalamu wa lishe” alisema Mhe Mayeka.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Chunya amekemea imani potofu zinazotokana na baadhi ya watu wakiwepo baadhi ya viongozi wa dini kuhusu afya zao huku akiwataka kutumia akili zao wenyewe au panapobidi wapate ushauri kutoka sehemu sahihi
“Ukikuta mafundisho yana kukataza kwenda hospitali kimbia eneo hilo maana sio salama na sisi serikali tunachukua hatua kwa watumishi wa namna hiyo na hata sasa kuna mtumishi (Mchungaji) mmoja tunamshikilia kwa kueneza imani potofu pia Niwapongeze wanaume wote mliojitokeza katika Mafunzo kuhusu lishe yatakayotolewa na wataalamu wa Afya na niwape pole na kuwashangaa wanaume wote wanaofikiri suala la lishe ni la mama peke yake bila kujua mtoto akipata udumavu familia nzima itakosa utulivu wa uzalishaji mali na hata wakati mwingine mtoto kuwa na uelewa mdogo awapo shuleni hivyo zingatieni miongozo ya lishe kama mnavyoelekezwa na watalamu wa lishe” Alisema Mhe. Mayeka
Afisa Maendeleo ya Jamii Vincent Msolla kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya amewataka wananchi kupeleka watoto kliniki ili wapate ushauri sahihi kutoka kwa watalamu wa Afya kuliko kusibiri tatizo litokee kwa mtoto ndipo wajitokeze Jambo linalofanya watumie muda mrefu kumuhudia mtoto huyo na hata serikali pia kutumia fedha nyingi
“Mahudhuria ya watoto kliniki sio mazuri kabisa na hilo sio jambo jema kwa mtoto mwenyewe na hata kwa familia hivyo tuhasishane kupeleka watoto kiliniki” Alisema Msolla
Awali akitoa salamu mbele ya Mgeni rasmi Mganga Mkuu wa wilaya Daktari Darison Andrew amesema bado wananchi hawajitokezi ipasavyo kuleta watoto wao kupata Chanjo kwani Halmashauri ya wilaya ya Chunya ina watoto elfu sabini (58,411) lakini ni watoto elfu arobaini na moja tu ( 41,000) wanaofika katika vituo vya afya kupata Chanjo
“Tuna watoto wengi hawapati chanjo, Tunatamani wazazi wa kiume wawe sehehumu kuleta watoto wao kupata Chanjo, tunao watoto elfu hamsini na nane lakini ni watoto elfu arobaini na moja tu wanaopata Chanjo”
Siku ya Afya na Lishe huadhimishwa kila baada ya miezi mitatu ambapo kila kijiji kinatakiwa kuadhimisha siku hiyo na Mkuu wa wilaya katika kila hafla ya siku za lishe kwa vijiji mara nyingi hufika na kuzungumza na wananchi kuhusu umuhimu wa lishe kama alivyofanya leo katika Kijiji cha Isnagawana.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S. Mayeka (Aliyeshika kikombe chekundu) akipata ufafanuzi hatua mbalimbali zilizotumika kutengeneza uji wa lishe katika siku ya Afya na Lishe kijiji cha Isangawana
Baadhi ya Wananchi Wa kijiji cha Isangawana wakiendelea na Darasa la uandaaji wa Uji wa Lishe katika siku ya Afya na Lishe
Mhudumu wa Afya ngazi ya jamii Ndugu Emily Kifubasi akielezea makundi mbalimbali ya vyakula kwa Mkuu wa wilaya akiongozana na viongazi mbalimbali wa wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.