Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka Saimon Mayeka amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Chunya kuwa serikali itaendela kushirikiana na viongozi wote wa dini bila kujali utofauti wa dini hizo katika kuhakikisha maendeleo ya wananchi waliopo wilayani Chunya Yanafikiwa huku akiwakumbusha kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina Dini lakini serikali inatambua kwamba wananchi wake wana dini
Ametoa kauli hiyo mapema jana wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi, Mbunge pamoja na marafiki wengine iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) jioni ya tarehe 19/04/2023 ambapo waislamu pamoja na watu mbalimbali walialikwa kushiriki
“Madhehebu ya dini yamekuwa na mchango Mkubwa sana katika maendeleo ya nchi hii hasa katika maeneo ya maadili. Sisi kama serikali hatusiti kushirikiana na nyinyi hasa kwa wilaya ya chunya, kwani wananchi wa Chunya wanahitaji kupata mafundisho yaliyomema na kuenenda kama mwenyezi MUNGU alivyowatarajia”
Mkuu wa wilaya pia amewataka wananchi wote wilayani Chunya kwa kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha tunarudi kwenye maadili yetu ya awali huku akiwasisitiza utandawazi ni mzuri kama ukitumiwa vizuri na masema tusipoangalia katika eneo hili la malezi iko siku tutapata viongozi wasio na maadili
“watoto zamani walikuwa watoto wa jamii nzima lakini hapa katikati mambo yameharibika hivyo turudi kwenye maadili yetu ya zamani, tusipoangalia haitashangaza kukapata viongozi wasio kuwa na maadili” alisema Mayeka
Akizungumza Mbele ya Mkuu wa wilaya Kaimu sheikh Mkuu wa wilaya ya Chunya, Sheikh Abdallah Mush amemshukuru Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Chunya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Lupa kwa namna walivyoona ni vema kuandaa futari kwaajili ya waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wote waliojumuika katika futari hiyo ya pamoja
“Namshukuru mwenyeezi MUNGU aliyetujalia kupata futari ya pamoja na ndugu zetu wote waliojumuika katika futari hii ya pamoja, ama hakika nitoe shukrani nyingi kwaniaba ya waislamu wa Chunya, Hatuna cha kukulipa ila mwenyeezi Mungu Atakulipa, Pia amewashukuru viongozi wa dini nyingine waliojumuika katika futari ya pamoja”
Akiwawakilisha waumini wa madhehebu ya dini ya kikristo Mch Lyos K. Mwalyosi ambaye ni mweneykiti wa jukwaa la wakristo wilayani Chunya amesema kwa niaba ya waumini wa dini ya kikristo wilayani Chunya kwamba wanamuwakilisha vema mkuu wa wilaya na amesema wao wako pamoja naye katika kila hatua ili kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Chunya wanapata maendeleo
“Niseme wazi tu mkuu wa wilaya pasina shaka tunakuwakilisha vizuri na tuko pamoja” alisema Mchungaji Mwalyosi
Kaimu Sheikh Mkuu wilaya ya Chunya Sheikh Abdallah Mush Akitoa Shukrani kwa Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi , Ofisi ya Mbunge pamoja na Wadau mbalimbali kwa kuandaa futari kwaajili ya waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wote waliojumuika katika futari hiyo ya pamoja
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.