Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka Simon Mayeka amesema namna bora ya kukabiliana na Majanga Mbalimbali katika maisha ya kawaida ya wananchi wilayani Chunya wakiwepo wakulima wa Tumbaku ni kuwa na Bima, Jambo ambalo litasaidia pale yanapotokea majanga yanayoweza kusabisha Mkulima kushindwa kuvuna Mazo yao vizuri
Mhe: Mayeka amesema hayo Jana wakati alipowatembelea wakulima wa zao la Tumbaku walio athiriwa na Mvua ya Mawe iliyonyesha mapema wiki hii ambapo zaidi ya ekari 90 zimeharibiwa katika vyama vya msingi vya Lupatinga tinga na Mtande ambapo karibu kilo laki moja zinakadiriwa kuharibiwa na mvua hiyo
“Kwanza miwapeni pole wakulima wote mliokumbwa na kadhia hii ya Mvua ya Mawe, kweli tumeona ni uharibifu Mkubwa ambao umefanywa namvua hii, Pamoja na uharibifu huu, Ni muhimu sasa wakulima tuanze kufikiria kukata Bima, wakulima hawa waliopata uharibifu huu tungekuwa tunashuhudia sasa wakipata fidia kupia bima zao kuliko hali hii tunayoishuhudia sasa”
Mkuu wa wilaya amewata viongozi wa vyama vya msingi vya tumbaku kuanza kufikiria uwepo wa mfuko wa maafa kwa wakulima wa zao la Tumbaku ili yanapotokea mambo kama haya basi mfuko huo utumike angalau kumsaidi mkulima ambaye amekumbwa na kadhia hiyo, huku akiwata chama kikuu cha Msingi kuchua hiyo kama agenda kuanza kuzungumza kwenye vikao
Pia amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kutafuta njia mbadala ya kuwasaidia wakulima waliopata madhara kutokana na mvua ya mawe ili waweze kuwalipa wafanyakazi waliokuwa wamewaajiri kwa msimu huu kwani kwasasa wakulima hao hawana namna tena ya kuwalipa wafanyakazi hao kutokana na mazao ambayo yalikuwa tegemeo lao kuharibiwa na mvua ya mawe.
Kwa Mujibu wa Afisa Kilimo wilaya ya Chunya Ndugu MWINUKA amesema bado wanaendela kufanya tathimini ya uharibifu wa mvua hiyo katika wilaya nzima na pindi itapokuwa imekamilika basi taarifa rasmi itatolewa idadi ya ekari zilizoathirika katika wilaya nzima pamoja na kilo zinazokadiriwa kupotea kutokana na uharibifu huo
Meneja wa bank ya CRDB tawi la Chunya na Afisa uhusiano wa Banki ya Azania tawi la Mbeya waliambatana na Mkuu wa wilaya, wamewasisitiza wakulima kuhakikisha wanakata Bima ili angalau kupata fidia ya uharibifu unaokuwa umejitokeza pale changamoto kama hii inapojitokeza huku wakisisitiza kwamba karibu kila mwaka walimu wamekuwa wakishuhudia uharibifu wa tumbaku kutokana na Mvua ya mawe
Akiwa katika ziara hiyo hiyo Mhe. Mayeka amepitia kukagua maendeleo ya ujenzi wa Sule ya Sekondari ya wasichana Mayeka inayojengwa katika Kata ya Lupatinga Tinga ambapo amehimiza kukamilishwa mapema hatua ya ujenzi iliyopo sasa ili wakaguzi wafike kukagua kiwango cha ujenji huo ukilinganisha na thamani ya fedha zilizotolewa kwaajili ya ujenzi kwa hatua hiyo.
“Mumalize ili tuje kukagua tuone thamani ya mradi kama inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa kwani hatuwezi kuleta fedha zingine bila kufanya ukaguzi na kujiridhisha kwamba ujenzi unaoendelea unakidhi viwango stahiki” amesema Mhe Mayake
Mhe. Mayeka pia alitembelea ujenzi wa jengo la abiria katika kituo cha Mabasi Lupa na kuwataka watumiaji wa jengo hilo kutumia kama lilivyokusudiwa na kuwataka wamiliki wa mabasi kutumia kituo hicho tofauti na ilivyosasa ambapo bado kuna baadhi ya mabasi bado yanatumia ujanja ujanja kushusha na kupakia abiria eneo ambalo sio kituo cha mabasi.
Mkuu wa wilaya amehitimisha ziara yake kwa kuzungmza na baadhi ya wanachama wa chama cha ushirika cha Mtande ambapo kwanza amewapa pole kwa uharibifu huo lakini pamoja na kusisitiza suala la bima kwa wakulima pia amehimiza wazazi kuendela kuwasimamia watoto kusoma kwa bidii pamoja na kushirki katika ujenzi wa Taifa huku akisema maendleao ya Taifa la Tanzania ni kwa faida ya wanajamii wenyewe
Ziara hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo kwa taarifa za uharibifu Mkubwa wa zao la Tumbaku uliotokana na Mvua kubwa ya mawe wilayani humo ambapo wakulima kumi na sita (16) kutoka chama cha ushirika cha Lupatinga tinga na wananchama kumi na tisa (19) kwa Chama cha ushirika Mtande wamepata athari kutokana mvua hiyo huku tathimini ikiendela kwa vyama vingine
Mwenyekiti wa chama Cha Ushirika Mtande, akielezea kiwango cha uharibifu wa Tumbaku mbele ya Mkuu wa wilaya alipotembelea kujionea uharibifu katika zao la Tumbaku kutokana mvua ya mawe
Moja ya Mashamba yaliyopata uharibifu kutokana na Mvua ya mawe
Afisa kilimo wilaya Chunya Ndugu Curthbet Mwinuka na Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika Cha Lupatinga tinga Ndugu Jilala (Mwenye suti nyeusi) walioinama chini wakifafanua Jambo mbele ya Mkuu wa wilaya Chunya alipotembelea kuona uharibifu wa mvua ya mawe kwa wakulima wa Tumbaku
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.