.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka ameitaka Divisheni ya Afya kufanya Ukaguzi wa mazingira ya nje na ndani katika zahanati zote zilizopo wilaya ya Chunya na kuhakikisha zinakuwa safi.
Ameitoa kauli hiyo jana tarehe 6 September 2023, wakati alipotembelea zahanati za Igundu na Godima, ambapo amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Darson Andrew kuhakkikisha anatembelea Zahanati zote za Wilaya Ya Chunya kukagua hali ya usafi wa Mazingira ya nje na ndani lakikini pia kuhakikisha taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na utunzaji mzuri wa kumbukumbu za dawa zinazoingia na kutoka
‘’Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) hakikisheni mnatembelea zahanati zote zilizopo wilaya ya Chunya na kukagua usafi wa mazingira ya nje na ndani lakini pia kuona kama taratibu na Miongozo mbalimbali inafuatwa na kuzingatiwa kulingana na taratibu zenu “ alisema Mhe. Mayeka
Mhe Mayeka pia amewataka wafanyakazi katika zahanati hizo kuhakikisha wanazingatia taratibu za kazi ikiwa ni pamoja na utunzaji wa kumbukumbu na kuhakikisha mazingira wanayofanya kazi yanakuwa katika hali ya Usafi kwaajili ya usalama wao na wagonjwa wanaokwenda kupata huduma katika zahanati hizo.
Kwaniaba ya Divisheni ya Afya ndugu Edward Tengulaga ambaye ni Mfamasia wa wilaya ya Chunya amesema wamepokea maagizo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha wanatembelea mara kwa mara zahanati kukagua kuhimiza suala la usafi wa mazingira pamoja na kufwatilia kuona kama taratibu zinafwatwa na kuzingatiwa
Mmmoja wa wagonjwa aliekuwa amefika katika Zahanati ya Godima kwaajili ya kupata Huduma ya matibabu ndugu Ester Razaro amesema kuwa anafurahishwa na hali ya usafi wa mazingira katika Zahanati hiyo pamoja na Huduma nzuri zinazotolewa .
Pamoja na Ukaguzi huo Mhe Mayeka amempongeza ndugu Orida Kassian Mtabibu wa zahanati ya Godima kwa Utunzaji Mzuri wa Kumbukumbu na kufuata Miongozo pamoja na Taratibu zilizowekwa, aidha amemtaka aendelee kufanya kazi kwa bidii na ufanisi zaidi na kuhakkikisha wanaendelea kutoa Huduma bora kwa wagojwa wanaofika zahanati hiyo kwaajili ya kupata huduma .
Ndugu Agrey Mroso Mtabibu wa Zahanati ya Igundu akimuonyesha jambo Mkuuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka wakati alipotembelea Zahanati hiyo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.