Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka amewataka maafisa usafirishaji (waendesha Badoboda, maguta pamoja na bajaji) na wananchi waliojitokeza kuwa wazalendo wenye kuipenda wilaya yao ya Chunya na Nchi kwa ujumla wake kuhakikisha wanashiriki kikamilisha katika masuala ya usalama
Ametoa kauli hiyo mapema jana wakati akikabidhi zawadi kwa timu ya Yanga A iliyoibuka mshindia wakati wa kuhitimisha mashindano ya Mayeka Usalama Cup yalitamaatika jana katika uwanja wa mpira wa miguu Sabasaba ambapo timu ya Yanga A iliwafunga timu ya Simba A gori moja kipindi cha kwanza gori lililoduma dakika zote tisini na kuifanya Yanga kuwa Mabingwa wa Mashindano hayo
“Michezo ni urafiki, michezo ni upendo, Mimi ninaamini mtatusaidia pia kwenye uslama wa wilaya yetu tunatamani kuwa na vijana ambao ni wazalendo mnatamani kuiona Chunya inaendelea Pamoja na mashindano leo kuisha tutapanga na viongozi wenu twende Hospitali ya wilaya, mkoa ili tukaone wenzetu ambao walipata madhira kupitia kazi hii ya usafirishaji na hii itatusaidia na sisi kuendelea kuchukua tahadhari”
Mhe Mayeka aliwapongeza timu ya Yanga kwa ushindi walioupata huku akisema mashindano haya kwa mwaka huu yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa lakini mwaka ujao mashindano hayo yataratibiwa kwa namna nyingine bora zaidi hivyo amewataka vijana hao kujiandaa na kuendeleza upendo kupitia michezo
“Niwapongeze Yanga kwa kushinda leo,, Mimi kwakweli ni kama mzazi mimi yeyote angeshinda kati yenu nafurahi ingawa Mimi ni ni samba, Hiki kilichofabnyika hapa tumefanya yanga na samba lakini lengo ni kupata wachezaji baadaye tutakuwa na timu moja na ndomaana niliwambia msikamiane sana ili msiumizane kwani baadaye mtakuwa timu moja na mashindano haya tulitaka kuona wachezaji na tumewaona kwa mimi nawapongeza sana”
Awali akitoa salamu la Jeshi la Polisi wilaya ya Chunya Mkuu wa polisi wilya ya Chunya SSP Nestory M John amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Chunya kwa kuandaa mashindano ya Mayeka usalama Cup yenye lengo la kuhimiza maafisa usafirishaji kuzingatia usalama wao kwanza na baadaye usalama wa abiria wake huku akihimiza kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya watu wenye nia ovu kwa wilaya ya Chunya pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi tu wanapokuwa na mashaka na abiria.
“Sisi kama upande wa jeshi la polisi tumefurahi na tumerizishwa na namna mlivyojitokeza na mlivyoshiriki.Ujumbe umefika na tumejikumbusha kuhusu Bima, usalama wetu kwanza, namna tunavyobeba abiria wetu tuwe makini na abaria hao maana wengine ni waharibifu na sisi wenye tuzingatie alama za barabarani tusizidishe spidi”
Mashindano ya Mayeka Usalama Cup yametamatika jana kwa michezo miwili ambapo mchezo wa Mapema ulihusisha timu za Simba B ikicheza na Yanga B kusaka mshindi wa Tatu na Timu ya Simba B iliibuka kidedea kwa gori moja na Baadaye Mchezo wa Fainali ambapo Yanga A ilicheza na Simba A matokeo ya gori moja yakaipatia Ushindi timu ya Yanga.
Wachezaji wa timu ya Yanga A wakiwa wameketi chini na nyuso za furaha baada ya kupata ushindi dhidi ya Simba A katika mashindano ya Mayeka Usalama Cup
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S.Mayeka akimkabidhi kombe Kapteni wa timu ya Yanga A iliyopata ushindi katika mashindano ya Mayeka Usalama Cup katika Uwanja wa mpira wa miguu Saba saba
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S.Mayeka akimkabidhi kombe Kiongozi wa timu ya Yanga A kiasi cha Tshs 100,000/= katika mashindano ya Mayeka Usalama Cup katika Uwanja wa mpira wa miguu Saba saba .
Timu ya Simba Awakiwa wameketi chini kwaajili ya shamlashamla zilizokuwa zikiendelea katika uwanja wa Mpira wa miguu Saba saba baada ya mchezo kumalizika
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.