Mkuu wa wilaya ya chunya Mhe Mayeka Saimon Mayeka amewataka walimu kuvitumia na kuvitunza vizuri vishikwambi walivyokabidhiwa ili vidumu kwa muda mrefu na kuendelea kurahisisha majukumu yao ya kila siku
Mayeka amesema hayo mwisho mwa wiki katika hafla ya kukabidhi vishikwambi kwa walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani chunya hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri (SAPANJO)
Afisa Elimu Msingi Ndugu Ferd Mhanze amemhakikishia Mkuu wa wilaya kwamba mafunzo kwa walimu kuhusu matumizi ya vifaa hivyo tayari yameanza na hata bajeti ijayo imezingatia hilo
Kwa niaba ya walimu waliopokea vishikwambi hivyo Mwalimu Jeras Shitindi Na Mwalim Wema Mwangolombe wamesema vifaa hivyo vitawasidia sana kwanza kurahisisha majukumu yanayohitaji TEHEMA, na walimu kujifunza Zaidi kuhusu TEHEMA kwani ulimwengu wa sasa unategemea Zaidi TEHEMA
Vishikwambi 594 vimekabidhiwa kwa walimu wa shule za msingi na sekondari zote zilizopo wilayani chunya ili kurahisisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.