Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani chunya chini ya mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe, Mayeka Simon Mayeka amewataka wananchi wa wilaya ya chunya kuhakikisha wanafuata kanuni, taratibu na sheria za nchi katika maeneo yao kwani bila Amani maeneo yetu hayatatawalika na hata shughuli za kiuchumi zitashindwa kufanyika
Amesema hayo mwisho wa juma wakati akiongoza kamati hiyo kukagua miradi ya maendeleo inayofanyika katika kijiji cha sipa kata ya Kambikatoto na baadaye kuongea na wananchi wa kijiji hicho ambapo amesema kijiji hicho kilikuwa na mafanikio makubwa sana jambo ambalo lilikuwa linapelekea kuwa na vigezo vya kuwa kata lakini wasipozuia mambo ya hovyo, yanayofanywa kinyume na sheria za nchi wanaweza kusabibisha kuporomoka kabisa
“Kuna kikundi kinaitwa wazee sijui wazee wa mila wao wanaona wako juu ya sheria na wanataka wao ndo wafanye maamuzi na nasikia kuna vikao vinafanyika porini, sasa ni marufuku kufanya vikao porini, vikao vyote vya kijiji vina utaratibu wake, Vikao vya kijiji vifanyike kwa utaratibu na vifanyike hadharani uongozi ujue vikao hivyo akiwepo mweshimiwa Diwani”
Aidha Mhe Mayeka amewataka viongozi wa serikali maeneo mbalimbali wilayani Chunya kuhakikisha mazao yanauzwa na kununuliwa kwa uataratibu uliowekwa na serikali lakini pia vipimo vinavyotumika viwe vipimo halali, na amewakumbusha kwamba Makamu wa Rais alishatoa mwongozo kwamba Lumbesa hazikubaliki na mazao yauzwe na kununuliwa kwa kilo.
“Mtendaji vipimo hivi havikubaliki kabisa, vinamuumiza mkulima, Viongozi wetu walishaagiza kazi yetu ni kutekeleza. Mazao yapimwe kwa mizani na sio kuuzwa kwa vipimo mbalimbali kama debe na vinginevyo”
Amewataka wananchi wa Chunya kuheshimu mpango wa matumizi bora ya ardhi wa mwaka 2007 ambao umeweka wazi maeneo ya makazi, maeneo ya malisho, maeneo ya hifadhi, maeneo ya mapitio ya wanyama pamoja na maeneo mengine mengi kulingana na matumizi husika, kwani kuendelea kukaa katika maeneo hayo ni kujiandalia hasara yako ya baadaye
“Mimi nawambia inawezekana mwaka jana ulikaa, mwaka huu unakaa hatujui mambo ya kesho, lakini muda utafika utatoka katika maeneo hayo, Tukishasema hili eneo la shoroba (Mapitio ya wanyama) basi ondokeni, tukisema eneo hili ni hifadhi au eneo hili sio la makazi ni la malisho ya mifugo basi msijenge nyumba za kudumu hapo kwani kuendelea kuishi na kujenga makazi ya kudumu katika maeneo hayo ni kujitakia hasara ya baadaye kwani muda utafika ambao utaondolewa kwa lazima”
Mkutano huo wa hadhara ulitanguliwa na kikao cha ndani ambapo kamati hiyo ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ambapo Mambo mbalimbali yalijadiliwa na baadaye kamati hiyo kupitia mwenyekiti wake iliwataka viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana, kwa uwazi na kwa umoja bila kujali kabila, dini na hata eneo ambalo mtu ametoka
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.