Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara wilayani Chunya amewata Watumishi wa Umma na wale wa Taasisi binasfi pamoja na Wafanyabiashara kushirikiana kuifanya wilaya ya Chunya kuwa Eneo salama la Biashara na uwekezaji ili kuwavutie wafanyabiashara wengi na hata wawekezaji kuja kuwekeza Chunya
Akizungumza kwenye kikao cha Barza la Biashara kilichoketi tarehe 2/6/2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) amesema upande mmoja ukitambua nafasi ya upande mwingine itasaidia kufanikisha biashara ya upande mmoja na kufanya hivyo lengo la serikali ya awamu ya sita ya kuletea ajira kwa wananchi wake, kuwainua wafanya Biashara na kuwatelea huduma bora wananchi wake linatimia kwa urahisi
“Wafanyakazi wa Serikali shirikianeni na wafanyabiashara kuhakikisha wanafanikiwa katika kazi zao kwani wako wananchi na wanachunya kwa ujumla wamejiajiri kupitia biashara na wameajiri watu wengine wengi hivyo mnapotaka kuwafungia biashara zao mfikilie watu wengine wanaofaidika kupitia biashara husika” amesema Mayeka
Aidha Mhe Mayeka ameongeza kusema kuwa kwa kipindi ambacho atakuwepo wilayani Chunya atahakikisha wafanya kazi wa serikali wanakuwa rafiki kwa wafanya baishara jambo ambalo litaongeza idadi ya wafanyabaishara, ambao kupitia biashara zao serikali itakusanya kodi ambazo zitatumika maeneo mbalimbali ya huduma kwa wananchi wa Chunya
“Kwa Muda ambao Mungu atanijalia kuwepo Chunya, Natamani kuona wafanyabiashara na Taasisi zote zinazowahusu wafanyabiashara kuwa na uhusiano mzuri Jambo ambalo litasaidia kuwainua wafanyabiashara wengi ambapo baadaye Makusanyo ya kodi yataongezekana lakini pia watu wengi watapata ajira nyingi na hatimaye maisha yao kubadilika kutokana na vipato hivyo”
Kupitia kikao hicho wafanyabiashara kwa nyakati tofauti wametoa kero wanazokumbana nazo wawapo katika biashara zao na kero kubwa ni watumishi wa Halmashauri kuchelewesha kutoa huduma, wakati mwingine kutokuwepo ofisini kipindi ambacho wafanyabiashara wanapohitaji huduma mbalimbali
Josia M Nandi (Mmiliki wa nyumba za starehe) yeye alisema “Kufanyike utaratibu mzuri wa namna ya ulipaji wa kodi kwa Vinywaji nje ya hapo tutaonekana wafanyabiashara wa huduma hizo hatutaki kulipa kodi, hivyo ni muhimu suala hilo litazamwe vizuri”
Lukas Malangalila yaye alijikita katika changamoto ya vizuizi vya mazao alisema “Shughuli zinazojitokeza kwenye vizuizi (Mageti) mbalimbali ni ngumu na zina usumbufu mkubwa kwa wafanya biashara. Nikuombe ukae vizuri na watu wa halmashauri ili warekebishe hilo”
Akijibu moja ya hoja walioitoa wajumbe wa Kikao hicho waliotaka kujua changamoto inayokwamisha ujenzi wa kituo cha Mabasi wilayani Chunya, Afisa rasilimali watu ndugu John Maholani akimuwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya chunya alisema
“Tayari taratibu za awali za ujenzi wa kituo hicho cha mabasi zimeanza kwani tayari mkandarasi mshauri wa kazi amepatikana ambaye ni Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia (MUST) na tayari wamewasilisha mchoro wa kwanza na sasa hivi karibu watakuja kuleta mchoro wa mwisho na taratibu nyingine ziendelee hivyo ni hivi karibu ujenzi wa kituo hicho cha Mabasi utaanza” alisema Maholani
Afisa Biashara wilaya ya Chunya Bw. Rodrick Mwakisole alipata nafasi ya kutoa elimu kwa ufupi kuhusu Mfumo mpya wa kukusanya mapayo (TAUS) kwamba nimfumo rahisi na rafiki kwa wafanyabiashara kwani wanaweza kufanya malipo yoyote kutoka eneo walilopo bila kufika katika ofisi za Halmashauri
“Mfumo umetengenezwa na watanzania wenyewe jambo ambalo litarahisisha kufanya marekebisho pale itakapotakiwa kufanya hivyo na mfumo huu ni rahisi kwakuwa taratibu zote za kuomba leseni na hata kulipia tozo mbalimba mteje anaweza kufanya bila kufika ofisi za halmashauri jambo ambalo litapunguza gharaza za usafiri kwa mteja” amesema Mwakisole
Kikao cha Baraza la Biashara huketiwa mara mbili kwa mwaka jambo ambalo husaidia kutatua Changamoto mbalimbali zinazowakumba wafanyabaishara, Wakuu wa idara wa halmashauri ya wilaya ya Chunya na Jeshi la Polisi walipata nafasi ya kujibia hoja zilizotolewa na wafanyabiashara na hoja nyingine zinazohitaji mchakato kupata majibu zinaendelea kushughulikiwa ili katika kikao kijacho zitatolewa ufafanuzi wa hatua zilizo chukuliwa
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka Akizungumza jambo katika kikao cha Baraza la Biashara
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.