Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka amewakemea watumishi wanaotumia muda wa serikali kufanya shughuli zao binafsi jambo linalopelekea kushuka kwa tija ya utumishi na utendaji wao kwani wanaoathirika ni Wananchi wanaotakiwa kuhudumiwa na watumishi katika maeneo mbalimbali ya wilaya
Ametoa kauli hiyo tarehe 18/9/2023 katika ukumbi wa mikutano Sapanjo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vilivyotolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maafisa ugani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ili kurahisisha utendaji kazi wao na baadaye kuleta Tija kwa wananchi na Tanzania kwa ujumla wake .
“Tutagombana mkiacha kufanya kazi za serikali mkaegemea kazi zenu binafsi muda wa kazi, Hivyo Nendeni mkafanye kazi vinginevyo mvivu ataonekana tu. Serikali inachotaka toka kwenu ni Tija yaani uwepo wako afisa kilimo na afisa mifugo uonekane kupitia kazi sio wakulima wanalima bila tija, wafugaji wanafuga bila tija na wewe upo tu maeneo hayo sasa kazi yako ni nini?” alisema Mhe. Mayeka
Mhe ,Mayeka amemtaka mkuu wa divisheni ya Kilimo na Mifugo wilaya ya Chunya kuandaa vigezo vya kuwapima maafisa hao na kuandaa ziara ya kukagua maeneo yao ya mfano kwani ni vigumu afisa mifugo kutokuwa na mifugo na hata afisa kilimo kutokuwa na shamba, hivyo ameagiza kuandaliwa kwa ziara maalumu ya kupita kukagua mifugo na mashamba ya maafisa hao
“Tutaandaa ziara maalumu ya kupita kukagua shamba la afisa kilimo lisilopungua heka moja pamoja na kukagua mifugo kwa afisa mifugo maana haiwezekana afisa kilimo hauna shamba na afisa Mifugo hauna mifugo” alisema Mhe. Mayeka
Naye Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Ndugu Cuthberth Mwinuka akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya amesema zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo ni mwendelezo wa serikali kuwasaidia maafisa hao ili kutekeleza majukumu yao jambo ambalo litaleta tija kwa mwananchi moja kwa moja kwani awali serikali iligawa vifaa vya usafiri kama vile Pikipiki lakini leo imeendeleza zoezi hilo kwa kuleta vifaa vingine
“Zoezi hili Mhe Mkuu wa wilaya ni mwendelezo kwani awali serikali ilitupatia vyomba vya usafiri ili kurahisisha maafisa hawa kufika maeneo mbalimbali ya kazi lakini sasa imetuongezea vifaa vingine ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Majukumu yetu ya kila siku” alisema Ndugu Mwinuka
Afis kilimo kata ya Sangambi ndugu Raymond Choga na Afisa ugani kata ya Matundasi ndugu Shani Ngoma kwa niaba ya wenzao wameishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyowajali huku wakiahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuhakikisha wanawahudumia wananchi katika maeneo yao na kwa kufanya hivyo wanasema waatakuwa wametimiza azma ya serikali
Vifaa vilivyogawiwa kwa maafisa kilimo na mifugo kwa kata zote za wilaya ya Chunya ni pamoja na Buti, koti, Pumpu Kompyuta, printa pamoja na kipima udogo (Soil scanner) Tableti pamoja na karatasi Maalumu (Transparency).
Mkuu wa Wilaya Mhe. Mayeka akimkabidhi buti , koti la mvua na pamp Afisa kilimo wa kata ya Maundasi ndugu Shani Ngoma
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka aliesimama katikati kwenye picha ya pamoja na maafisa kilimo na mifugo wa kata za halmashaui ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.