Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mheshimiwa Mubarak Alhaji Batenga amewataka wananchi wa kijiji cha Masiano wilayani Chunya waliovamia eneo la mradi la kilimo cha Soya kuondoka kwenye eneo hilo mara moja ili kupisha utekelezaji wa mradi wa kilimo cha zao la Soya utakaotekelezwa na serikali hivi punde kupitia udhamini wa benki ya dunia.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara kijiji cha Masiano, Septemba 19, 2024, Mheshimiwa Batenga amesema wananchi wote waliovamia eneo la mradi wa kilimo cha Soya katika kijiji cha Masiano kilichopo Wilayani Chunya kuondoka .
“Waliovamia eneo la mradi wanapaswa kuondoka na Serikali itawapa kila kaya heka 50 pamoja na hati miliki katika eneo lililopo msitu wa kijiji ili kupisha utekelezaji wa mradi huu mkubwa wa kilimo cha Soya”, amesema Batenga.
Mhe. Batenga aliongeza kuwa, wananchi wa Masiaono na Mapogolo ndio wanufaika wa kwanza mara baada ya mradi wa kilimo cha Soya kuanza kutekelezwa huku akiwataka vijana kujipanga vyema kushiriki kwenye mradi huo ili kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Batenga amesema kupitia mpango bora wa matumizi ya ardhi, Serikali imetenga eneo lenye ekari 2594 lililopo kijiji cha Mapogolo na Shoga kwaajili ya wafugaji wa Kijiji cha Masiano na Mapogolo ambapo Serikali itapanda majani kwaajili ya malisho, kuchimba mabwawa ya maji upatikanaji na kujenga majosho ya mifugo.
“Wananchi wa kijiji cha Masiano munapaswa kuheshimu mpango bora wa matumizi ya ardhi ambao mumeupitisha kupitia mikutano yenu ya kijiji na mpango huu mumeuhuisha kulingana na mahitaji yaliyopo sasa, kuwa na matumizi bora ya ardhi kutaondoa migogoro ya ardhi pamoja na serikali kuweza kuwaletea wananchi maendeleo” amesema DC Batenga.
Kwa upande wa wananchi wa kijiji cha Masiano walimueleza Mhe. Batenga changamoto zilizopo kwenye kijiji chao ikiwemo ubovu wa barabara, kutokukamilika kwa madarasa ya shule na upungufu wa madawati, ukosefu wa nishati ya umeme, upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na kutokuwepo kwa zahanati kwenye kijiji hicho ambapo serikali imeahidi mwaka huu wa fedha kuzipatia ufumbuzi wa haraka.
Mhe. Batenga yupo kwenye ziara yake ya kawaida ya kukutana na wananchi kwa kila kijiji kusikiliza kero zao na kutatua. Wakati wa mkutano huu Mhe. Batenga amewakikishia wananchi kuwa kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa wananchi wake kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi, mradi wa kilimo cha Soya utakapoanza, Serikali itapeleka huduma zote muhimu za kijamii ikiwemo kuchonga barabara, huduma ya umeme na maji, kujenga zahanati, kujenga shule na huduma nyingine zote za kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Masiano kilichopo kata ya Chokaa
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Masiano waliojitokeza kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mkuu wa wilaya ya Chunya ili kupeleka Kero zao zipatiwe ufumbuzi
Moja kati ya wananchi wengi waliojitokeza kutoa kero za kijiji chao Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga wakati wa Mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga akisikiliza na kuandika kero za wananchi wakati wa Mkutano wa Hadhara kwenye kitongoji cha Masiano kilichopo kijiji cha Mapogoro kata ya Chokaa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.