Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaj Batenga ametoa rai kwa wananchi na kinamama wajawazito kuhakikisha wanazingatia ulaji wa vyakula ambavyo vimezingatia misingi ya lishe ili kuboresha afya ya mwili na akili lakini pia kujiepusha na maradhi mbalimbali yanayotokana na ulaji mbovu kama vile udumavu na utapiamlo kwani wasipokula lishe bora basi wataishia kula dawa kama lishe.
Kauli hiyo ameitoa leo Octoba 30/2024 wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Lishe Kitaifa ambapo kiwilaya maadhimisho hayo yamefanyika kata ya Matundasi katika viwanja vya Shule ya Msingi Matundasi.
“Tunasema tunazingatia lishe lakini ni muhimu kwa kina mama wajawazito kuzingatia mnakula nini mnapokuwa na mimba lakini pia hata ukijifungua kuzingatia unakula nini ili yule mtoto naye anaponyonya aweze kunyonya mlo kamili kupitia maziwa na hiyo ndio lishe vinginevyo watoto hao itakuwa shida huko tunako kwenda bila kujua kwamba tatizo lilianzia wapi kumbe tatizo lilianza na wazazi wenyewe pale ambapo hatukuwapa lishe ya kutosha pindi wakiwa tumboni mpaka wanakuja kuzaliwa”.
Mhe.Batenga pia amezungumzuia suala la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024 huku akiwaagiza watoto wote kuwahimiza wazazi wao na ndugu zao kwenda kupiga kura siku hiyo kwani ni haki yao ya kidemokrasia ya kuwachagua viongozi wanaowataka.
“Tarehe 27 Novemba ikifika itakuwa siku ya mapunziko ninyi wanafunzi hamtakuja Shule hivyo nawatuma watoto wote siku hiyo muwakumbusha baba, mama dada kaka na wengine wenye miaka 18 na zaidi wakapige kura nyinyi mtabaki nyumbani siku hiyo mkilinda nyumba ili wazazi waende wakapige kura na kuwachagua viongozi wao wanao wataka” alisema Batenga
Naye kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya ndugu Ryoba Kebasho amesema kuwa suala la Lishe linaanza kabla mtoto hajazaliwa yaani pale ambapo wazazi wanapanga mipango ya kupata mototo ili kumjenga mtoto atakaepatikana kuanzia akiwa tumboni mwa mama yake.
Vilevile, Daktari Kebasho amesisitiza wakinamama wajawazito kupatiwa elimu kuhusu lishe na afya ili kujenga kizazi cha kesho kilicho bora na kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza kwa kukosa lishe.
“Mama kabla hajapata ujauzito anatakiwa kula lishe bora ili kuanza maandalizi ya kujenga mtoto atakaepatikana baadae kuanzia akiwa tumboni na baada ya kuzaliwa ikiwa ni pamoja na kutumia virutubisho vinavyotolewa katika vituo vya afya kwani mtoto asipopatiwa lishe bora hawezi kukuwa vizuri kimwili na kiakili “alisema Ryoba.
Maadhimisho ya siku ya Lishe kitaifa hufanyika tarehe 31 Oktoba ambapo kwa mwaka huu Wilaya ya Chunya yamefanyika katika kata ya Matundasi huku yakiwa yamepambwa na burudani mbalimbali zilizobebe jumbe kuhusu lishe chini ya kauli mbiu isemayo Mchongo ni Afya yako, Zingatia unachokula.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga akizungumzia umuhimu wa Lishe wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Kitaifa ambapo wilayani Chunya Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Matundasi kata ya Matundasi .
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitalli ya Wilaya ndugu Ryoba Kashebo akielezea namna ambavyo elimu ya Lishe imekuwa ikitolewa katika jamii wakati wa Maadhimishao ya siku ya Lishe viwanja vya Shule ya Msingi Matundasi kata ya Matundasi
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Matundasi wakitoa elimu kuhusu lishe kwa njia ya burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Matundasi.
Wnanafunzi na wazazi waliojitokeza wakati wa Maadhimisho ya siku ya lishe yaliyoodhimishwa katika viwanja vya Shule ya msingi Matundasi wilayani Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.