Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga ameagiza Shule zote wilayani Chunya kuwa na Mashamba yasiyopungua hekari kumi ili mazao yatakayopatikana yatumike kama chakula kwa wanafunzi jambo ambalo litawaondolea wazazi na walezi mzigo wa kuchangia huku akiagiza Maafisa Ugani kusimamia Mashamba hayo vizuri ili kuwawezesha wananchi wengine kuja kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo chenye manufaa.
Maagizo hayo ameyatoa leo wakati aliposhiriki kikao cha kamati ya Lishe cha Robo ya pili kwa mwaka 2023/2024 kilichoketi leo tarehe 16/2/2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya uliopo jengo jipya la utawala.
“Tunakwenda kutengeneza mashamba darasa katika shule zetu zote wilayani Chunya. Shule ziwe na Mashamba yasiyopungua heka kumi (10) na mazao yanayopatikana yatumike kwaajili ya chakula shuleni na maafisa ugani wa kata wasimamie mashamba hayo, Kwakufanya hivyo lile lengo la kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika utekelezaji wa mkata wa Lishe litafanikiwa” Amesema Mhe Batenga
Katika nafasi nyingine amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa juhudi kubwa anazofanya katika kusimamia utekelezaji wa mkataba wa lishe ambapo kupitia juhudi hizo wilaya ya Chunya kw mara tatu mfululizo imeshika nafasi ya tatu kitaifa katika utekelezaji wa mkataba wa Lishe
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona amewataka Idara tumizi na simamizi kwa ujumla kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwaajili ya utekelezaji wa afua za lishe zinatumika kama ilivyokusudiwa kwani yeye katika ofisi yake ni kuhakikisha fedha zinapatikana lakini kazi ya kusimamia iko chini ya Idara zinazohusika kutumia na kusimamia fedha hizo
“Hatutaki taarifa za mwisho zinakuja zinaeleza eneo Fulani tuna asilimia 99.9 au asilimia chini ya hapo, sisi tunachotaka kila eneo kama miongozo inavyoelekeza tunafikia asilimia 100 na kama tunaruhusiwa hata Zaidi lakini sitaki kuona tuko chini ya asilimia 100 eneo lolote la utekelezaji wa mkataba wa Lishe, naomba idara simamieni hili”
James Sunge kaimu Mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii, Mw Abdalah Mchelu kaimu mkuu wa idara ya elimu ya Awali na Msingi, Mw Konzeta Ngachenga kaimu mkuu wa idara ya elimu Sekondari na Nicholaus Chambala kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha robo ya pili pamoja na mikakati yao kuhakikisha kile kilichokusudiwa kinafikiwa kwa wakati na kwa weledi
Kikao cha kawaida cha kamati ya lishe wilaya ya Chunya kimeketi leo tarehe 16/2/2024 kikiwa na lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mkataba wa lishe kwa Robo ya pili jambo ambalo hutoa dira juu ya kinachoendelea kufanyika katika kipindi cha Robo ya tatu ikiwa ni pamoja na kurekebisha panaoonekana kukwamisha utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.
Afisa lishe wilaya ya Chunya Bi Rehema Hiluka akifafanua jambo wakati wa kikao cha Lishe Robo ya pili ya mwaka 2023/2024 kilichoketi mapema leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo jengo jipya la utawala Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Mganga mkuu wa wilaya ya Chunya Dr Darison Andrew akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa mwaka ulipopita mbele ya Mkuu wa wilaya mapema leo wakati wa kikaao cha Lishe robo ya pili ya mwaka 2023/2024
Kaimu mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu James Sunge akijibu hoja wakati wa kikao cha kamati ya Lishe baada ya kumaliza kuwasilisha taarifa ya idara hiyo juu ya utekelezaji wa afua za Lishe
Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu ya awali na Msingi wilaya ya Chunya Mw Abdalah Mchelu akifafanua namna ambavyo idara itahakikisha agizo la shule la kuwa na mashamba namna litakavyotekelezwa katika idara ya Elimu ya awali na msingi
Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu sekondari Mw Konzeta Ngachenga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe zilizofanywa na Idara ya elimu sekondari kwa Robo ya pili ya mwaka 2023/2024
Wajumbe wa kamati ya Lishe wakiwa kwenye kikao cha Lishe kwa Robo ya pili ya mwaka 2023/2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo Jengo jipya la Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.