Mkuu wa wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mhe Mbaraka Alhaji Batenga ameagiza uongozi wa Kipembawe Saccos kuitisha Mkutano mkuu ndani ya mwezi mmoja ili kuhakikisha wananchama wote wanashiriki kikamilifu katika maamuzi yoyote watakayoona yanafaa kwa manufaa ya Kipembawe Saccos
Agizo hilo limetolewa jana tarehe 6/2/2024 katika Mkutano Mkuu maalumu ulioketi ukumbi wa Alfani Lupa ambapo lengo la mkutano huo ilikuwa kusomewa taarifa ya mwenendo wa Kipembawe Saccos baada ya wajumbe kutokuwa na taarifa yoyote kutoka kwa uongozi kwani ni Zaidi ya miaka miwili mkutano mkuu haujaitishwa
“Afisa Ushirika simamia hili ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo tarehe 6/2/2024 mpaka tarehe 6/3/2024 mkutano mkuu uitishwe na taarifa za mkutano huo zitolewe wiki mbili kabla ya mkutano na mkutano huo lazima uhudhuliwe na Zaidi ya asilimia 75 ya wanachama. Katika taarifa zenu mtakazo wasilishwa kwa wanachama wenu lazima ziwe wazi na zijumuishe taarifa ya watu mnao wadai, dhamana zao zikoje, sifa za kukopeshwa zilikuwaje na mambo mengine, maafisa ushirika wasaidieni viongozi kuandaa taarifa ambazo zitakidhi matakwa ya wananchama” Alisema Mhe Batenga
Aidha Mhe Batenga aliwataka viongozi na wanachama wa Kipembawe Saccos kuhakikisha wanakuwa Mabalozi wazuri wa Saccos yao ili watu wengine walio nje ya Saccos hiyo wavutike kuwa wanachama kwani uhai wa Saccos yoyote ile ni uwepo wa idadi kubwa ya wanachama na kama wanachama wanapopungua ni dalili ya kufa kwa Saccos
“Ni kazi kwetu sote kuhakikisha watu walio nje ya Saccos yetu waipende Saccos na wajiunge ili uhai wa Saccos uendelee maana uhai wa Saccos yoyote ile ni uwepo wa Idadi kubwa ya wanachama ambao wanajiunga kila mwaka au kwa kipindi ambacho Saccos wanaweza kupanga kupokea wanachama wapya” Alisema Batenga
Mjumbe wa Bodi ya Kipembawe Saccos ndugu Biniford Andrew Matola kwa Niaba ya viongozi wenzake wa bodi alikili wazi kukiuka kanuni na taratibu zinazoongoza Saccos yao kwa kushindwa kuitisha mkutano mkuu kwa karibu miaka miwili huku akisema hawakuwa na lengo lolote baya juu ya Saccos hiyo bali changamoto mbalimbali ndizo zilikuwa kikwazo cha wao kushindwa kuitisha mikutano hiyo
Awali akitoa taarifa kwa wajumbe wa Mkutano huo maalumu katibu wa Kipembawe Saccos ndugu Aman Daniel Hussein lengo la Saccos hiyo ilikuwa ni kuwana na Zaidi ya wanachama 800 lakini kwa sasa ina wanachama 105 akitaja sababu iliyopelekea kuwa na idadi hiyo ya wanachama ni changamoto zilizojitokeza za kuyumba uzalishaji wa zao la Tumbaku jambo lililopelekea hata wanachama kuyumba kiuchumi
Ndugu Aman Daniel Hussein Katibu wa Kipembawe Saccos akisoma taarifa Mbelaya ya Mkuu wa wilaya na wajumbe walio Hudhuria kikao hucho Maalumu
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.