Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga ameonya wananchi wa wilaya ya Chunya kuwaficha watoto wenye mahitaji maalumu jambo linalopelekea watoto hao kukosa huduma na haki zao za msingi anazostahili kuzipata ikiwepo haki ya kupata Elimu, haki ya kupendwa na haki ya kupatiwa mahitaji yote muhimu kama watoto wengine
Ametoa onyo hili tarehe 18/6/2024 katika viwanja vya ofisi ya kata ya Ifumbo wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila tarehe 16 Juni ya kila mwaka lakini Halmashauri ya wilaya ya Chunya wameadhimisha siku hiyo tarehe 18/6/2024
“Kuna watu wanaficha watoto wenye mahitaji maalumu, wanawanyima watoto hao kupata haki yao ya kupata elimu, Serikali imetoa fedha ya kujenga shule mbalimbali kwaajili ya watoto wenye mahitaji maalumu, Chunya tunazo Shule ya Msingi Kibaoni, na shule ya Msingi Makonglosi hivyo wapelekeni watoto shule wapate Elimu. Tunaposherehekea siku ya mtoto wa Afrika hatutaki kumwacha mtoto yeyote nyuma, wote wote wakasome bila kujali changamoto alizonazo” Alisema Mhe Batenga
Aidha Mhe Batenda amewataka viongozi wa dini wilayani Chunya kutumia majukwaa yao kuwaongoza waumini kuhakikisha wanapinga ukatili kwa watoto kwani viongozi hao wa dini wanayo nafasi kubwa na muhimu kuhakikisha ukatili unatokomezwa wilayani Chunya na kwakufanya hivyo watakuwa wametimiza lengo la kuwa na dini mbalimbali katika maeneo yetu
“Viongozi wa dini ni wapeleka ujumbe wazuri sana kwa jamii yetu, hivyo niwaombe viongozi wa dini kufikisha ujumbe kwa watu tunaowaongoza wa kukemea vitendo vya ukatili kwa watoto na hiyo ndiyo ibada sahihi kwa miongozo ya dini zetu” Aliongeza Mhe Batenga
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya Bi Twijisye Ephraim aliwataka wananchi wa Ifumbo kutumia maadhimisho hayo kuunganisha nguvu pamoja ili kukemea na kupinga ukatili wanaofanyiwa watoto katika mazingira yao na kwakufanya hivyo watakuwa wanalinda Taifa la kesho
“Lengo la maadhimisho haya kufanyika kila mwaka ni sisi wananchi kujitathimini kwa pamoja na kuunganisha nguvu kwa pamoja ili Tutafute suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo watoto bila kujali mtoto huyu ni wako au si wako au mtoto huyu analelewa na nani kwani watoto wote ni watoto wa Taifa zima la Tanzania na ni watoto wetu sote kama jamii” alisema Bi Twijisye
Akitoa salamu za wananchi wa kata ya Ifumbo Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya, Diwani wa kata ya Ifumbo Mh. Weston S. Mpyila aliwataka wananchi wa Ifumbo kutowafanyisha kazi kupita kiasi watoto lakini amewataka kuongeza upendo kwa watoto wao ili kuwasaidia kufikia ndoto zao
“Niwasihi wananchi wenzangu tusiwafanyishe kazi wototo wetu kupita kiasi, lakini pia niwaombe kuanzia leo watoto wetu tuwapende na tuwapeleke shule watoto na hili siwaombi maana ni suala la lazima na ndio maana Serikali inajenga miundombinu mbalimbali ya Shule ili watoto wapate elimu, wananchi naomba yote yanayozungumzwa hapa tuyafanyie kazi”Alimesema Mhe Mpyila
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila tarehe 16 Juni ya Kila mwaka yakiwa na lengo la kufanya tathimini na kuchukua hatua katika kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi bila vizuizi vyovyote. Kwa mwaka huu maadhimisho hayo yaliongozwa na kauli mbiu “Elimu jumuishi kwa watoto, Izingatie Maarifa, Maadili na Stadi za kazi”
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga alizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ifumbo mapema tarehe 18/06/2024
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya Bi Twijisye Ephraim akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kata ya Ifumbo
Diwani wa kata ya Ifumbo Mh. Weston S. Mpyila akitoa salamu za wananchi wa kata ya Ifumbo Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika kata ya Ifumbo kwenye viwanja vya ofisi ya kata ya Ifumbo
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga amkikabidhi Juisi Bi Elizabeth Conrad Lusale afisa kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii ili aendelee kuratibu ugawaji wa juisi hizo pamoja na Biscut kwa watoto wote waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
Watoto kutoka Blac Maendeleo Kids wakighani Shairi Mbele ya Mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kata ya Ifumbo katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Watoto kutoka moja ya vikundi vilivyotumbuiza katika madhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, wakiimba kwa huzuni namna haki za watoto zinavyokandamizwa huku wakipeleka ombi lao kwa jamii kujaliwa maana wao ni Taifa la Kesho
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga akimkabidhi vifaa vya Shule Mwanafunzi mmoja kwa niaba ya wanafunzi wengine Saba waliopatiwa vifaa vya Shule ikiwa ni kuendeleza azma ya Serikali ya kuwajali wananchi wake pamoja na kutoa somo kwa wananchi wengine kuendelea kuwajali watoto wote bila kuwabagua kulingana na hali zao
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.