Mkuu wa wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mhe Mbarak Alhaji Batenga amesema kazi kubwa atakayofanya kwa kushirikiana na viongozi wengine waliopo wilayani Chunya ni kuhakikisha wanaenda kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ili wananchi wa Chunya waendelee kuiamini serikali yao
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 22/12/2023 kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chunya wakati alipokabidhiwa rasmi ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya na mtangulizi wake Mhe Mayeka S Mayeka ambaye amehamishiwa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ambako anaenda kuwa Mkuu wa wilaya hiyo
“Kazi kubwa tuliyo nayo ni kuhakikisha watu hawalalamiki na ikitokea wananchi wanalalamika basi sisi hatujafanya kazi yetu hivyo naomba tujipange kwenda kwa wananchi kusikiliza kero zao na kuzipatia majibu ili wananchi hao waendelee kuiamini serikali waliyo ichagua”
Mhe Matenga amemtaarifu Mkurugenzi mtendaji kuwahimiza wahandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi ya maendeleo kwani moja ya maeneo yatakayopewa kipaumbele kikubwa ni utekelezaji wa miradi ya maendeleo maana serikali ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingin kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali yenye lengo la kuwasogezea huduma wananchi
Awali akitoa taarifa ya wilaya ya Chunya mbele ya Mhe Batenga, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Chunya ambaye sasa ni mkuu wa wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S Mayeka amesema viongozi wote wa wilaya ya Chunya wanaushirikiano mkubwa na bila shaka viongozi hao watampatia ushirikiano unaotakiwa mkuu wa wilaya ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi ipasavyo
“Ushirikiano uliopo kati ya Ofisi ya Mkuu wa wilaya na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji umefanya Wilaya ya Chunya kufanya vizuri maeneo mbalimbali kimkoa na kitaifa na jambo hilo tayari tumekuabiliana kwamba nafasi ya tatu kitaifa katika utekelezaji wa mkataba wa Lishe sasa inatosha, tunatafuta nafasi ya kwanza kitaifa na hilo linawezekana kama mkishirikiana vizuri”
Makabidhino hayo ya ofisi yanakuja ikiwa ni siku chache zilizopita baada ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mabadiriko ya vituo vya kazi kwa wakuu wa wilaya kadhaa ambapo amembadilishia kituo cha kazi Mhe Mayeka S Mayeka kutoka wilaya ya Chunya na kwenda wilaya ya Kongwa na pia amembadilishia kituo cha kazi Mhe Mbarak Alhaji Batenga kutoka wilaya ya Kiteto mkoani Manyara na kuja kuwa Mkuu wa wilaya ya Chunya.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mhe Mbarak Alhaji Batenga akizungumza wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya yaliyofanyika mapema leo
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka (Aliyenyoosha kidole) akizungumza Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama wakati wa makabidhiano ya ofisi mapema leo
Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya Chunya wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao cha Makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.