Katibu Tawala wilaya ya Chunya ndugu Anackleth Michombero amewataka na kuwasisitizia wasimamizi wa miradi ya SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement) kuhakikisha shamani zinazotumia mbao kama vile milango na madawati zitengenezwe kwa mbao zilizokauka vizuri ili zisipoteza ubora wa Mradi kwani wakitumia mbao mbichi zitakapokauka zinaweza kupasuka na kupoteza ubora wa thamani hizo.
Ametoka kauli hiyo jana terehe October 12, 2023 wakati alipotembela na kukagua miradi hiyo katika kata ya Lualaje na Kambikatoto na kujionea halihalisi ya ujenzi inavyoendelea ambapo mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kambikatoto upo hatua ya upauaji wakati mradi wa Ujenzi wa nyumba ya walimu (2 in 1) upo hatua ya upauaji na upigaji wa plasta.
Pia Katibu tawala amewapongeza wasimamizi wa miradi ya SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement) kwa hatua ya ujenzi wa miradi ilipofikia katika ujenzi wa Shule ya Sekondari kambikatoto wenye thamani ya Shilingi Milioni miatano themanini na tatu (583.180.028) pamoja na Ujenzi wa nyumba ya walimu yenye uwezo wa kubeba familia mbili (2 in1) katika shule ya Sekondari Lualaje yenye thamani ya shilingi milioni miamoja (100.000.000).
‘’Nawapongeza sana kwa hatua hii ya ujenzi mliyofikia mmefanya kazi nzuri hongereni sana lakini mjitahidi kukimbizana na muda kwa hatua zilizobaki ili kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati huku mkiendelea kuwashirikasha wananchi kwa sehemu ambazo mnahitaji nguvu za wananchi” alisema Michombero
Naye Afisa elimu Vifaa na takwimu halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Costansia Komba amepokea maelekezo ya katibu tawala na kuwataka wasimamizi wa ujenzi walioko eneo la miradi hiyo kuhaikisha wanawatembelea mara kwa mara wazabuni wao ilikuhakiki ubora wa malighafi zinazotumika kutengenezea thamani za milango na madawati.
Awali akisoma taarifa Afisa elimu kata wa kata ya Kambikatoto ndugu Msana Mahona amesema kuwa kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa mpaka sasa imechangiwa na nguvu kubwa ya wananchi ambapo ni pamoja na kusafisha eneo la ujenzi, kulipa fidia eneo la ujenzi, kubeba mchanga, kokoto, mawe na kifusi mbayo ni sawa na million 45,035,000 na kuongeza kuwa wananchi bado wanaendelea kushiriki katika ujenzi wa mradi huo.
Nae afisa elimu kata wa kata ya Lualaje ndugu Evaristo Kayeta amesema kuwa wananchi wameshiriki katika mradi huo kwa kiasi kikubwa ambapo jumlaya million 10,914,000 ni nguvu ya wananchi iliyotumika mpaka hatua ya mradi ulipofikia sasa nabado wananchi wanaendelea kujitolea nguvu kazi mpaka mradi utakapokamilika.
Katika kutembelea na kukagua miradi ya SEQUIP Katibu tawala pia alitembelea shule mpya ya Kipembawe iliyojengwa katika kijiji cha Mafyeko kata ya Mafyeko kupitia mradi wa BOOST ambapo ujenzi wa Shule hiyo umekamilika yamesalia mambo madogomadogo ambayo wanaendelea kuyakamilisha.
Katibu tawala Ndugu Anakleth Michombero akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Kambikatoto iliyopo kata ya Kambikatoto akiwana na baadhi yawasimamizi wa mradi huoBaadhi ya majengo ya madarasa Shule ya Sekondari Kambikatoto kupitia mradi wa SEQUIP
Nyumba wa walimu shule ya Sekondari Lualaje iliyojengwa kupitia mradi wa SEQUIP yenye jumla ya vyumba 6 ikiwa na uwezo wa kubeba familia mbili (2 in 1)
Katibu Tawala aliyekaa dawati la kwanza upande wa kulia kwenye picha ya pomoja na baadhi ya wasimamizi wa mradi wa BOOST Shule mpya ya msingi Kipembawe iliyojengwa kata ya Mafyeko walipokuwa wakikagua madawati hayo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.