Katibu tawala Wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero amewataka maafisa mifugo kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na kuwafikia wafugaji wengi kwa wakati ili kuhakikisha lengo la serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwahudumia wananchi wote wakiwepo wafugaji linatimia ipasavyo
Amesema hayo alipokuwa akikabidhi pikipiki kwa maafisa mifugo kutoka katika kata 6 za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambapo zoezi la kukabidhi pikipiki hizo lilifanyika katika Jengo la jipya la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Usafiri huu ukawe chachu ya kuleta mabadiliko katika utendaji kazi wenu, tuone kabla hamjawa na vyombo vya usafiri na baada ya kuwa na vyombo vya usafiri utendaji wenu uwe na mabadiriko, tunatarajia kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya kuwafikia na kuwapa huduma wafugaji wote” alisema Michombero
Aidha amewataka maafisa Mifugo hao kuhakikisha vitendea kazi hivyo vinatumika kwa manufaa ya serikali ili kuwahudumia wananchi katika maeneo yao huku akiwakumbusha kuzingatia usalama wao wakiwa wanaendesha pikipiki hizo kwani wakienda kinyume vitendea kazi hivyo vinaweza kusababisha ulemavu na wakati mwingine hata kugharimu maisha
“Vyombo hivi makavitumie vizuri mkivitumia vibaya vinaweza vikawasababishia ulemavu lakini pia mkavitumie kwa matumizi ya serikali na kwa matumizi mengineyo” alisema Michombero
Awali akisomaa taarifa fupi kwa katibu tawala, Mkuu wa idara ya kilimo na mifugo ndugu Cuthbert Mwinuka amemshukuru mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwawezesha maafisa mifugo ili kuwarahisishia kuwafikia wananchi (wafugaji) katika maeneo yao
Wakizungumza kwa niaba ya Maafisa mifigo wengine Bi Witness Judika wa kata ya Mamba na Godfrey Katamba wa kata ya Kambikatoto wamemshukuru Rais na serikali kwa ujumla kwa kuwapa vyombo vya usafiri (Pikipiki) kwani vitaongeza ufanisi na kurahisisha utendaji kazi wao lakini pia vitawasaidia kuwafikia wafugaji wengi kwa wakati tofauti ilivyokuwa awali walipokuwa hawana vyombo vya usafiri.
Hii ni awamu ya pili ya ugawaji wa pikipiki kwa maafisa Mifugo ambapo awali ziligawiwa pikipiki 2 kwa kata ya Chokaa na kata ya Kasanga na awamu ya pili zimegawiwa pikipiki 6 katika kata ya Mamba, Kambikatoto, Mafyeko, Lualaje, Nkung’ungu, na Sangambi na kufanya jumla ya pikipiki 8 .
Vitendea kazi (pikipiki) vikiwa vimepaki kwaajili ya kukabidhiwa kwa Maafisa mifugo kutoka katika kata 6 za halmashURI ya Wilaya ya Chunya
Maafisa Mifugo wakiwa na vitendea kazi (pikipiki) walivyakabidhiwa kwaajili ya kuvitumia katika kutekeleza majukumu ya serikali
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.