Afisa tawala wa wilaya ya Chunya Bi. Semwano Mlawa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya amezindua rasmi kampeni ya upandaji miti kiwilaya.
Zoezi hili limefanyika leo Februari 15, 2022 katika Shule ya Msingi Chunya Kati iliyopo kijiji cha Sijilili, kata ya Itewe huku ikiongozwa na kauli Mbiu isemayo, TANZANIA YA KIJANI INAWEZEKANA PANDA MITI KWA MAENDELEO ENDELEVU
Upandaji huo wa miti ni njia ya kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa hasa na ukataji wa miti unaopelekea kukosekana kwa mvua za kutosha hivyo kuathiri shughuli za maendeleo kwa wananchi.
“Ni vyema tushirikiane kwa pamoja kuchukua hatua kwa wanaoharibu mazingira, na sio kumuachia mtu au taasisi inayohusika na utunzaji wa mazingira, ni jukumu la kila mmoja wetu ikiwemo wananchi kulinda mazingira yetu.” Alisema Bi Semwano Afisa Tawala wilaya ya Chunya
Akisoma risala, Afisa Maliasili wa Wilaya ya Chunya Bi. Rehema P. Mwabulambo amesema, pamoja na wito wa upandaji miti bado kuna uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti na cchomaji moto ovyo.
Aidha aliongeza kwa kusema, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kupitia kampeni hii imefanikiwa kupanda miti kwa wastani wa hekta 200 – 250 wilaya nzima kwa mwaka.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Bw. Cuthbert Mwinuka amesema, zoezi la upandaji miti kwa Wilaya ya Chunya tayari ilishaanza kwa tarafa zote mbili za wilaya hiyo.
“Upandaji wa miti kwa Halmashauri ulianza tangu mvua za mwanzo zilipoanza kunyesha na ni zoezi enedevu,” alisema Mwinuka.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chunya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri.
Afisa Tawala wa Wilaya ya Chunya Bi Semwano akishiriki kupanda mti katika eneo la shule ya msingi Chunya kati.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bw Filex Maholani akishiriki kupanda mti katika eneo la shule ya msingi Chunya Kati
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bw. Cuthbert Mwinuka akishiriki kupanda mti katika eneo la shule ya msingi Chunya Kati.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.