Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeendeleza kuziongoza Halmashauri za Mkoa wa Mbeya katika ukusanyaji wa Mapato kwa tofauti ya zaidi ya asilimia arobaini (40%) baada ya kukusanya shilingi bilioni 7.3 sawa na asilimia 133 kwa kipindi cha Kuanzia julai mosi mpaka tarehe 23 februali 2024 huku Halmashauri ambayo inafuatia ikiwa na asilimia 90 ya makusanyo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya juu ya mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kuanzia julai mosi 2023 mpaka februali 23 Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa kipindi chote cha mwaka huu imeendelea kuongoza na kwa sasa inaongoza kwa tofauti ya asilimia arobaini (40%).
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya amekuwa kinara wa kuhimiza watumishi anaowaongoza kufanya kazi kwa weledi, kujituma na kwa uzalendo huku akiwataka kuheshimiana, kuheshimu kanuni na taratibu za utumishi wa umma jambo ambalo limekuwa chachu kubwa ya mafanikio ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya katika Nyanja mbalimbali ikiwepo ukusanyaji wa Mapato
Halmashauri ya wilaya ya Chunya itaendelea kuongoza Mkoa wa Mbeya katika ukusanyaji wa Mapato hata mwaka ujao yaani 2024/2025 kutoka hali ya zao la Tumbaku kuwa ya Kuvutia na kuridhisha Mashambani jambo linalotoa taswira ya Mafanikio makubwa ya mavuno ukilinganisha na mwaka jana yaani 2023/2024 ambapo Halmashauri ya wilaya ilikusanya Zaidi ya shilingi bilioni mbili kutokana na kilimo cha Tumbaku
Aidha kutokana na makusanyo yanayotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato Halmashauri ya wilaya imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali kupitia mapato yake ya Ndani, miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Shule ya Mchepuo wa Kiingeleza, Ujenzi wa Kituo cha afya sangambi na miradi mingine hivyo kuendelea kuimarika katika ukusanyaji wa mapato ni ishara tosha ya mwendelezo wa ujenzi wa miradi zaidi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya ili kuendela kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi katika maeneo yao
Halmashauri ya wilaya ya Chunya ilikadiliwa kukusanya shilingi bilioni 5.54 katika kipindi cha mwaka 2023/2024 lakini mapaka kipindi cha februari 23 mwaka 2024 ikiwa ni pungufu ya miezi 4 kufikia kipindi kilichokusudiwa Halmashauri ya wilaya ya Chunya tayari imekusanya shilingi bilioni 7.35 sawa na asilimia 133 ya lengo lililokusudiwa na kwa kiwango hicho Halmashauri ya wilaya ya Chunya imezizidi Halmashauri nyingine za mkoa wa Mbeya kwa tofauti ya zaidi ya asilimia arobaini (40%)
Wanachi mnaaswa kuendelea kuiamini na kuiunga mkoa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo kwa wilaya ya Chunya viongozi waliopo kila mmoja kwa nafasi yake wanamsaidia vyema Mhe Rais katika kuwaletea maendelea wananchi wake lakini pia shilikianane na viongozi hao ili kuijenga Chunya mnayoihitaji
Hali ya zao la Tumbaku kwa msimu huu wa kilimo katika mashamba mbalimbali katika mkoa wa Kitumbaku Chunya
Wakulima wakiwa katika ufungaji wa Tumbaku tayari kwa kuikausha baada ya kuivuna kutoka Mashambani wilayani Chunya katika msimu huu wa kilimo
Tumbaki ikiwa imekausha na imefungwa tayari kwa kupelekwa sokoni ili kuuzwa na hatimaye Mkulima wa wilaya ya Chunya aanze kupata matunda ya kazi yake ya kilimo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.