Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaj Batenga amesema kuwa serikali ya Wilaya ya Chunya inaungana na wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chunya kuunga mkono maamuzi yaliyofanywa na Mkutano Mkuu Maalum wa Chama wa kupitisha jina la Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa kuwa mgombea wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025, kwasababu ya utekeleza wa ilani ya CCM kwa vitendo ikihusisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kutatua kero za Wananchi.
Kauli hiyo ameitoa tarehe 24/01/2025 wakati akitoa salam za serikali mbele ya katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya katika hafla ya kumpongeza Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM kuwa Mgombea wa kiti cha Urais na viongozi wengine wa kitaifa .
“Tunazo sababu kama wananchi wa Chunya za kuunga mkono uamuzi wa mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, sisi kama serikali tulipewa ilani tukaitekeleza, Chama cha Mapinduzi ndio kimetupa ilani tukaitekeleza chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan, tunayo mambo mengi yamemefanyika katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwepo wa umeme katika vijiji na utekelezaji unaenda mpaka kwenye vitongoji, ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ,ujenzi wa uwanja wa kisasa na miradi mingine ya maendeleo na Wananchi wa Chunya wanaelewa”amesema Mhe. Batenga.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Frank Uwagire akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wanachunya amepongeza uongozi wa serikali ya Chunya kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa uwanja wamichezo wa kisasa, ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa na miradi mingine ambayo ni majibu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.
“Nitoe pongezi kwa serikali yaWilaya ya Chunya kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo leo inatufanya tunatembea vifua mbele ikiwemo ujenzi wa stendi mpya ya kisasa, ujenzi wa uwanja wa kisasa , soko la dhahabu la kisasa , na leo ukija Chunya unaikuta dunia yote iko Chunya kwasababu ya dhahabu , lakini pia makusanyo makubwa ya mapato mnapeleka kwenye miradi ya maendeleo, Chama Cha mapinduzi Mkoa wa Mbeya tunawapongeza sana “amesema Uwagire.
Aidha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Umoja wa Vijana CCM Wilaya(UVCCM), Umoja wa wanawake Tanzania(UWT) , Jumuiya ya Wazazi Wilaya, Baraza la wazee Wilaya na Wanachunya wametoa matamko yao yakuunga Mkono maamuzi yaliyofanywa na Halmashauri kuu na Mkutano Mkuu wa CCM wa kumpitisha mgombea urais na Viongozi wengine kwa ngazi ya kitaifa kutokana na kazi nzuri zilizofanywa na Dkt Samia pamoja na Viongozi wengine .
Hafla ya pongezi kwa Viongozi walioteuliwa kwa nafasi mbalimbali za kitaifa kupitia Chama cha Mapinduzi imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa serikali , Makundi mbalimbali ya Uongozi ndani ya CCM, na wananchi kupitia maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi kilichoketi Tarehe 18 na 19 Januari 2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo makao makuu ya nchi Dodoma.
Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya ndugu Frank Uhagile akizungumza na wanachama wa chama cha mapinduzi na Wanachunya waliokusanyika katika hafla ya kumpongeza dkt Samia suluhu Hassan kwa kupishwa na Mkutano Mkuu kuwa mgombea wa kiti cha urais .
Wanachama wa chama cha mapinduzi waliokusanyika katika hafla ya kumpongeza Dkt Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ( Sapanjo).
Wanachama wa chama cha Mapinduzi wakiwa kwenye maandamano kuelekea ukumi wa mikutano wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya ( Sapanjo) kwaajili ya hafla ya kumpongeza Dkt Samia Suluhu Hassan.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.