Halmashauri ya wilaya ya Chunya ikiwa ni moja na sehemu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshiriki maonesho ya utalii yenye jina “KARIBU KUSINI”yanayofanyika Mkoani Iringa yenye lengo la Kukuza utalii mikoa ya Nyanda za Juu kusini kwani mikoa hiyo ina vivutio vingi ambavyo havipatikani maeneo mengine
Halmashauri ya wilaya ya Chunya imewakilishwa na Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Chunya,Afisa Utalii wilaya ya Chunya Ndugu Petro Haule pamoja na afisa Biashara wa wilaya ya Chunya ndugu Sebastiana Mapinga wamesema maonesho hayo ni muhimu kwanza kubadilishana uzoefu na mbinu mpya zinazohusu utalii na hata kufungua fursa za kibiashara kupitia Utalii kwani Wilaya ya Chunya ina vivutio mbalimbali kama vile Bwawa la Viboko Zingwa matundasi, Kambi ya wapigania uhuru, Mlima Mwene na vingine ambavyo vinaweza kutumika kuvutia fursa za kibiashara
Akizungumza mbele ya wageni mbalimbali waliotembelea banda la maonesho la Mkoa wa Mbeya afisa utalii wa wilaya ya Chunya ndugu Petro Haule amesema Maonesho hayo yanamaana kubwa sana kwa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwani kupitia maonesho hayo watu Mbalimbali watakuja Chunya kuona vivutio hivyo na pia kuja kuwekeza katika fursa Mbalimbali za kibiashara
“Kupitia maonesho hayo sisi kama wilaya ya Chunya tumejifunza mambo mengi muhimu yanayohusu namna sahihi ya kutunza na kuhifadhi vivutio vyetu na hata miundombinu ya kuvifikia vivutio hivyo lakini sisi tuliowakilisha wilaya ya Chunya tumeona namna wenzetu walivyotumia fursa ya utalii kufungua biashara mbalimbali hivyo Chunya tunaenda kulifanyika kazi jambo hilo”
Wageni Mbalimbali wametembelea Banda la Mkoa wa Mbeya wakiwepo viongozi wa wizara, Mikoa na wilaya lakini viongozi na wadau wa Taasisi mbalimbali za serikali na taasisi zisizo za Kiserikali ambapo kwa asilimia kubwa wameonesha utayari wa kutembelea mkoa wa Mbeya na Fulsa zzinazopatikana kwenye sekta ya Madini wilayani Chunya imekuwa ni kivutio kikubwa kwa viongozi mbalimbali na wananchi waliotembelea Banda la Mkoa wa Mbeya
Maonesho ya Utalii yaliyopewa jina “KARIBU KUSINI” yanafanyika Mkoani Iringa, Manispaa ya Iringa eneo la Kihesa-Kilolo barabara ya kuelekea Dodoma, Maonesho hayo leo yamefikia siku ya nne na yanataraji kudumu kwa siku tano ambapo kilele cha Maonesho hayo itakuwa tarehe 27/9/2023
Afisa utalii Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Petro Haule akifafanua jambo mbele ya Viongozi Mbalimbali waliotembelea kuona vivutia vya utalii vilivyopo Mkoa wa Mbeya, Alye vaa shart la Kitenge ni Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Mbarali Missana Kalela Kwangula akisaini kitabu katika Banda la utalii Mkoa wa Mbeya wakati wa Maonesho ya KARIBU KUSINI
Afisa Utalii wilaya ya Chunya Ndugu Petro Haule akishirikiana na Afisa utalii wilaya ya Rungwe Ndugu Numwagile Bughali wakifafanua vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Mkoa wa Mbeya kwa Ujumla wake wakati wa maonesho ya utalii yanayoenda kwa jina la KARIBU KUSINI yanayoendelea mkoani Iringa
Baadhi ya Maafisa kutoka wilaya ya Chunya na Rungwe wakiwa juu ya moja ya kivutio cha Utalii (Daraja la MUNGU) ambapo maji ya Mto Ruaha mdogo yanapita chini lakini Juu kuna mawe. wa kwanza Kutoka Kulia ni Joshua Sengo (Afisa Habari wilaya ya Chunya) anayefuata ni Petro Haule (Afisa Utalii kutoka wilaya ya Chunya), Noah Kibona (Afisa Habari wilaya ya Rungwe na wa Mwisho ni Numwaghile Bugali (Afisa utalii wilaya ya Rungwe)
Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Utalii "KARIBU KUSINI" wakiwa kwenye picha ya Pamoja kwenye Kabuli la Mashujaa (LIGALU) Lugalo ya sasa eneo ambalo watanzania kupitia Chifu Mkwawa waliwashinda Wajerumani wakati wa harakati za Kupinga Ukoloni
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.