Halmashauri ya wilaya ya Chunya Chini ya viongozi wake Mahiri imerejea katika nafasi yake ya kwanza katika ukusanyaji wa Mapato mkoani Mbeya kwa kipindi cha Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 jambo ambalo kwa wilaya ya Chunya kwake ni kawaida kushika nafasi hiyo na kwa umahiri wa viongozi wake wilaya ya Chunya hakuna nafasi ya kurudi nyuma.
Serikali imekuwa na kawaida ya kutoa taarifa kwa wananchi wake juu ya mwenendo wa mambo mbalimbali yanayotekelezwa ili waweza kufahamu kinachofanywa na serikali waliyoiamini ambayo kwa sasa ni awamu ya sita ikiongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amejibainisha wazi kwamba ni Rais anayetaka uwazi na uwajibikaji kwa kila mtu kulingana na nafasi yake.
Wilaya ya Chunya Chini ya viongozi wake Mkuu wa wilaya Mhe Mayeka S. Mayeka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco S. Mwanginde, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim H. Kambona Pamoja na Mbunge wa Jimbo la Lupa wamekuwa wakishirkiana kwa ukaribu kuhakikisha kila linalotekelzwa Chunya linafanikiwa kwa kiwango kinachotakiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe hivi karibuni Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeongoza mkoa wa Mbeya kutekeleza zoezi la Chanjo ya Polia kwa zaidi ya asilimia mia moja na sitini (160%) na kufanikiwa kuziacha mbali halmashauri nyingine lakini pia ni hivi karibu wilaya ya Chunya imeshika nafasi ya Tatu kitaifa kutekeleza mkataba wa lishe kwa wananchi wake hivyo Chunya nafasi ya kwanza katika ngazi ya Mkoa sasa ni kawaida.
Kwa usimamizi mzuri toka kwa viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya, ushirikiano kwa watumishi pamoja na uwajibikaji kwa kila mtu kulingana na nafasi yake ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya ni hakika Chunya itaendelea kufanya vizuri Maeneo yote ndani ya Mkoa na hata ngazi ya Taifa.
Wananchi endeleeni kuiamini serikali ya awamu ya sita ili iendelee kutekeleza azma yake ya kuwatumikia wananchi wa wilaya ya Chunya na Watanzania wote kwa ujumla na msiache kulipa kodi na kufanya kazi za haki kama ambavyo serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inavyotaka wananchunya tuishi.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.