Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeendelea kuongoza mkoa wa Mbeya kwenye ukusanyaji wa mapato ambapo kwa sasa imefikia asilimia tisini na nane (98%) ya makusanyo ya mapato kulingana na makadirio yaliyokuwa yamewekwa hivyo kubakiza asilimia mbili ya makusanyo kufikia lengo la makadirio ya makusanyo kwa mwaka
Kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuhusu Mwenendo wa ukuanyaji wa mapato ya Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kuanzia tarehe 1 Julai mpaka tarehe 8 Desemba Halmashauri ya wilaya ya Chunya imekusanya asilimia tisini na nane (98%) ya Lengo la makusanyo ya mwaka 2023/2024 ambapo imekusanya bilioni 5.4 wakati ilipangiwa kukusanya bilioni 5.5
Aidha Halmashauri ya wilaya ya Chunya itaendelea kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali kwasababu ushirikiano uliopo kwa viongozi wote wa wilaya ya Chunya ukianzia ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya, Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, akiwawakilisha Madiwani wote wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Lupa, Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji pamoja na watumishi wote kwa ujumla umeimarika, Lakini pia usimamizi makini wa Chama Cha Mapinduzi unasaidia sana wilaya ya Chunya kufanya vizuri
Kwa kipindi cha Julai mosi mpaka Desemba 8, 2023 Halmashauri ya wilaya ya Chunya imekusanya shilingi bilioni tano na milioni mia nne na tano elfu laki nane na kumi na mia nane themanini na sita na sent tisini na nane (5,405,810.886.98) ambayo ni sawa na asilimia tisini na nane (98%) wakati ilikusudiwa kukusanya shilingi bilioni tano milioni mia tano arobaini na tatu laki tatu na hamsini na nane elfu (5,543,358,000.00)
Halmashauri ya wilaya ya Chunya imejipanga kuendelea kufanya vizuri maeneo mbalimbali kuanzia ngazi ya Mkoa na kitaifa na jambo hilo limekuwa likipewa msisitizo katika vikao mbalimbali na hata wananchi wa wilaya ya Chunya hushirikishwa ipasavyo jambo litakaloendelea kuwapa nafasi Halmashauri ya wilaya ya Chunya kufanya vizuri maeneo mbalimbali
Kupitia mapato yanayokusanywa na Halmashauri ya wilaya ya Chunya hupelekea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata na Vijiji mbalimbali vya wilaya ya Chunya, Mfano wa Miradi iliyotekelezwa kwa mapato ya Ndani ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Sangambi, Ujenzi wa Soko la Madini, Ujenzi wa Shule ya mchepuo wa kiingereza Chunya na miradi mingine mingi hivyo wananchi wa Chunya waendelee kushiriki katika ukusanyaji wa mapato ili mabadiriko makubwa ya utekelezaji wa miradi kupitia fedha zinazokusanywa.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.