Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njeru Kasaka amewata viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanatumia vizuri vifungu vinavyotakiwa kulipa stahiki mbalimbali za watumishi kuepuka kuisha au kubasti kwa vifungu hivyo jambo linalopelekea Halmashauri kushindwa kuwalipa watumishi wake wanapohitaji kulipwa jambo linaloongeza madeni kwa Halmashauri.
Ametoa kauli hiyo mapema tarehe 27/8/2024 wakati akitoa salamu kwenye kikao cha Baraza la Madiwani liloketi kujadili na kupitisha hesabu za mwisho wa mwaka 2023/2024 za Halmashauri ya wilaya ya Chunya kilichoketi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri uliopo jingo jipya la utawala.
“Tunatakiwa kujipanga kuona vipengele vyakulipa madeni havibust na kuweza kulipa malipo mbalimbali” alisema Kasaka.
Aidha Mhe. Kasaka aliongeza kuwa mambo mazuri yanayotokea ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya ni utekelezaji mzuri wa ilani ya Chama cha Mapinduzi huku akisema usimamizi mzuri wa Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na ushirikiano uliopo baina ya waheshimiwa Madiwani na Wataalam.
Pia Mhe Masache aliungana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa (LAAC) kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa maendeleo makubwa yaliyopo kwenye Wilaya hiyo.
“Mwanzoni wa mwezi Agosti, LAAC ilifanya kikao chake, pamoja na mambo mengine imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa kufanya vizuri kwenye ukusanya wa mapato na matumizi ya fedha za mapato hayo” alisema Kasaka.
Baraza la kujadili na kupitisha hesabu za mwisho za mwaka 2023/2024 za Halmashauri limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, Mbunge, Waheshimiwa Madiwani, Wataalam mbalimbali kutoka Halmashaui ,Wakuu wa Taasisi na Waandishi wa Habari.
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njeru Kasaka akizungumza Jambo wakati wa Baraza la kupitia hesabu za mwaka wa fedha 2023/2024 lililoketi mapema tarehe 27/08/2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya uliopo jengo jipya la wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.