Halmashauri ya wilaya ya Chunya kupitia kamati yake ya Mapamo kwa kushirikiana na wadau na wananchi wote wa wilaya ya Chunya inataraji kukusanya Shilingi Bilioni nane (8,747,616,000.00/=) kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ambao umeanza mapema Julai Mosi 2024.s
Akitoa ufafanuzi wakati wa kikao cha Mapato kilichoketi leo katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ulipo kwenye jengo jipya la utawala Mwenyekiti wa kamati ya Mapato wilaya ya Chunya Adv. Athuman Bamba amesema ili kufikia malengo ni lazima Halmashauri ikusanye milioni 125 kila wiki lakini pia vikao vya kila wiki vitasaidia kufanya tathimini wa mwenendo wa ukusanyaji wa Mapato hayo ili kubadili utaratibu na kuongeza nguvu ya ufuatiliaji pale itakapotakiwa kufanya hivyo
Wajumbe wa kikao hicho wamekubaliana kwamba kila mmoja mwenye jukumu katika usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kuhakikisha anatekeleza jukumu lake ipasavyo huku watendaji wa Kata wakitakiwa kuongeza juhudi katika maeneo yanayowahusu moja kwa moja.
Kupitia kikao hicho wajumbe wamepata wasaa wa kujadili kwa kina namna watakovyokusanya mapato katika vyanzo ambavyo vilikuwepo mwaka uliopita na vile ambavyo havikuwepo mwaka uliopita lakini mwaka huu vipo, Vyanzo ambavyo havikuwepo mwaka uliopita ila mwaka huu 2024/2025 vipo ni pamoja na Ada za Mabango,Kodi ya Majengo, Ushuu wa Maegesho ya Malori na Magari na Kodi ya pango la Ardhi.
Ikumbukwe mwaka wa fedha ulioisha hivi karibu 2023/2024 Halmashauri ya wilaya ya Chunya iliongoza Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kwa kipindi chote katika ukusanyaji wa Mapato jambo ambalo liliwezekana kutokana na Juhudi ya Kamati ya Mapato, watendaji ngazi mbalimbali pamoja na ushiriki Mzuri wa wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Kupitia Mapato ya Ndani Halmashauri imeendelea kutekeleza miradi Mbalimbali ikiwepo Ujenzi wa Kituo cha Afya Sangambi, Ujenzi wa Shule ya Mchepuo wa Kingeleza, Ujenzi wa Soko la Madini na kwasasa Ujenzi unaoendelea ni ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambapo pamoja na ushiriki mzuri wa wadau wa Maendeleo lakini pia Halmashauri ya wilaya ya Chunya nayo hushiriki kwa namna moja au nyingine katika kuchangia fedha lakini pia kuhakikisha Ujenzi huo unasimamiwa vyema na watalamu wake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mapato Halmashauri ya wilaya ya Chunya Adv Bamba (Aliyenyoosha Mkono Mbele) akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichoketi Mapema leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Jengo Jipya la utawala)
Afisa Biashara wa wilaya ya Chunya ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Mapato Ndugu Lodrick Mwakisole akizungmza jambo wakati wa Kikao cha Mapato mapema leo
Ndugu Paul Lugodisha ambaye ni afisa kilimo akichangia Jambo wakati wa kikao cha Mapato kilichoketi leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.