Shirika la TDFT chini ya mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili kwa ufadhiri wa watu wa Marekani wamefanikisha mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi sitini (60) wa Shule za Msingi na Sekondari zenye kutoka tarafa ya Kipembawe wilayani Chunya zenye Klabu za Uhifadhi wa wanyama pori, viumbe hai na utunzaji wa mazingira kwa ujumla (TAWA MALIAHAI KLABU) kwenda kujifunza uhifadhi wa wanyamapori, viumbe hai na utunzaji wa Mazingira katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Akifafanua kuhusu ziara hiyo meneja wa mradi Ndugu Samson Ipyana Mwakihaba amesema lengo la ziara hiyo ni kuwafundisha kwa vitendo wanafunzi wanachama wa klabu za uhifadhi wanyama pori, viumbe hai na utunzaji wa Mazingira kwa ujumla ili kwanza kuthibitisha walichojifunza kwa nadharia lakini pia kuongeza uelewa juu ya uhifadhi, na baadaye kuandaa mabalozi sahihi na wenye uelewa sahihi wa uhifadhi wa wanyama pori, viumbe hai na utunzaji wa mazingira kwa ujumla wake
“Tuko kwenye ziara kwa lengo la kuongeza elimu kwa vitendo juu ya Uhifadhi wanyapori, viumbe hai na mazingira kwa ujumla huku Lengo likiwa ni kuandaa mabalozi wazuri wa uhifadhi wa wanyama pori, viumbe hai na utunzaji wa Mazingira kwa ujumla na bila shaka watakuwa walimu wazuri kwa watu wengine hususani jamii inayowazunguka hivyo lengo la kuongeza Elimu juu ya uhifadhi wa wanyamapori, viumbe hai na utunzaji wa mazingira litakuwa limefanikiwa” Amesema Mwakihaba
Aidha Mwakihaba pamoja na kuishukuru Serikali ya Marekani kufadhiri mradi huo uliopelekea wanafunzi kupata ziara ya mafunzo kwa vitendo, pia ametaja Shue zilizonufaika na ziara hiyo ya mafunzo Shule ya Sekondari Mtanila (wanafunzi 10), Shule ya Msingi Matwiga (Wanfaunzi 10) Shule ya Msingi Mafyeko (wanafunzi 10), Shue ya Msingi Bitimanyanga (wanafuzni 10), Shule ya Msingi Kambikatoto (wanafunzi 10) na Shule ya Msingi Sipa (wanafunzi 10) hivyo kukamilisha idadi ya wanafunzi 60. Walimu wane kutoka Sipa, Matwiga, Bitimnyanga na Mtanila waliungana ili kuwasimamia wanafunzi hao
Afisa kutoka idara ya Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya ambaye alikuwa mmojawapo katika Safari hiyo Bi Jennifer Oscar amesema safari inafaida kubwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwani pamoja na kuongeza uelewa wa washiriki katika mambo ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira amesema wanafunzi wamepata burudani, wameongeza kuifahamu jiografia ya nchi yao hivyo kuendelea kukuza uzalendo ndani ya mioyo yao lakini inaongeza hamasa kwanza kwa washiriki wa safari na baadaye wanafunzi wengine nao watahamasika kushiriki kwenye uhifadhi wa mazingira wakijua iko siku nao wataenda kujifunza maeneo mengine mbali na nyumbani kwao
Ziara hiyo imedumu kwa siku tatu ambapo Martha Marko kutoka Shule ya Sekondari Mtanila, na Shabani Brown kutoka Shule ya Msingi Matwiga kwaniaba ya wanafunzi wengine wamesema wamefurahia safari hiyo huku wakishuhudia wanyama mbalimbali kwa ukaribu tofauti na ilivyokuwa hapo awali kwani kila kitu ilikuwa nadharia kwao na kupitia ziara hiyo wanafunzi wamekiri kuenda kuitumia vyema elimu waliyoipata ili kuhakikisha wanyamapori na viumbe hai wengine wanakuwa salama katika maeneo yetu
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.