Mkuu wa wilay ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka amesema endapo wananchi wa wilaya ya Chunya wataamua vema kama serikali inavyotaka basi wilaya ya Chunya itakuwa ni eneo la watu kuja kujifunza namna bora ya ufugaji wenye tija ambao utapelekea mifugo inayopatikana wilayani Chunya kuwavutia wanunuzi wengi jambo litakalo inua vipato vya wananchi kwa ujumla.
Mhe Mayeka ametoa kauli hiyo Jana July 4, 2023 alipokuwa anazungumza na wafugaji, wakulima kutoka kata ya Kambikatokto na Mafyeko pamoja na wataalamu kutoka Ngazi za vijiji, kata na halmashauri kilichoketi katika viwanja vya shule ya Msingi Bitimanyanga chenye lengo la kueleza mpanga wa serikali wa kuwatambua wafugaji ili wagawiwe maeneo ya malisho kulingana na idadi ya mifugo wanayomiliki.
“Kwa idadi ya mifugo tuliyonayo laki mbili na kitu, idadi ya watu kulingana na sensa ya 2022 ambapo Chunya ina watu laki tatu na arobaini hivi na eneo letu la mraba ambalo ni zaidi ya hekta elfu kumi na tatu tunaweza kuishi bila shida na mifugo yetu bila migogoro yoyote kati ya wafugaji na wakulima, hivyo ni muhimu tutambue wafugaji wetu wako wangapi, wana idadi gani ya mifugo ndipo tuwagawie maeneo yaliyotengwa kwa malisho ambapo serikali itapeleka mahitaji yote yanayohitajika kwa ufugaji bora”. Alisema Mhe. Mayeka
Mhe Mayeka amewataka watu wote waliovamia maeneo ya malisho yaliyotengwa kwa mujibu wa Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi wa mwaka 2006 kuanza kuondoka kwani serikali itapita kuhakiki maeneo hayo hivi karibuni na kuanza kuyatumia kama mpango wa matumizi bora ya ardhi unavyoelekeza na kwasasa maeneo hayo takwimu zinaonesha kuvamiwa kwa kiasi kikubwa
“Wakulima wote waliovamia eneo la malisho kwa mujibu wa Mpango wa Matumizi bora ya ardhi wa mwaka 2006 wajiandae kupisha kwani muda si mrefu maeneo hayo yatakuwa Ranchi za mifugo na wafugaji ambao wamejenga eneo la malisho kupunguziwa eneo hilo kulingana na idadi ya mifugo aliyonayo” alisema Mhe. Mayeka.
Afisa kilimo wilaya ya Chunya Ndugu, Cuthberth Mwinuka ametaja changamoto zinazokabili eneo la malisho ambapo amesema uvamizi wa maeneo ya marisho kutoka kwa wakulima lakini wananchi kujenga kwenye maeneo ya malisho pamoja na ongezeko la mifugo kwenye baadhi ya maeneo. Kuingizwa mifugo kihole hupelekea ugumu kupata idadi kamili ya mifugo
“Eneo la malisho linapungua sana jambo linalopeleka migogoro ya wakulima na wafugaji, changamoto kubwa ni maeneo ya malisho kuvamiwa na shughuli nyingine ikiwepo kulima, maeneo ya malisho kuwa na mifugo mingi kulinganisha na eneo jambo linalosababishwa na uingizaji hole kutoka nje ya wilaya na hata wakati mwingine ndani ya wilaya” alisema Mwinuka.
Julius Nguvumali, Abdalah Marijani na Bize Kefasi Kilongozi kwa niaba ya wajumbe wengine wa kikao hicho kwanza wameishukuru serikali kuja na mpango huo ambao utafanya wakulima kuwa huru katika shughuli zao na wafugaji kufuga kwa uhuru tofauti na ilivyo sasa, Pamoja na shukrani hizo wametamani kujua ni lini hasa zoezi hilo litanza huku wakitamani ikiwezekana iwe mapema sana na kila hoja waliyouliza imejibiwa palepale na Mkuu wa wilaya.
Kikao hiki kimekuja ikiwa ni mwendelezo wa kikao kilichowakutanisha wafugaji kutoka Tarafa ya kiwanja kilichoketi mapema wiki iliyopita ambapo lengo kubwa ni kuwafikia wafugaji wote ili kuwasiaidia waweze kufuga kwa tija tofauti na ilivyo sasa.
Mkuu wa wilaya Mhe. Mayeka akizungumza na wafugaji katika viwanja vya Shule ya msingi Biti manyanga
Afisa kilimo na mifugo wa Wilaya Ndugu Cuthbert Mwinuka akitoa taarifa ya mifugo mbele ya Mkuu wa wilaya na wajumbe wengine wa kikao
Ndugu Abdallah Marijani kutoka Kambi katoto akichangia katika kikao cha wafugaji kilichoongozwa na Mkuu wa wilaya
Ndugu Julius Nguvumali akichangia katika kikao cha wafugaji
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.