• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

CHUNYA YA AZIMIA KUTOA CHAKULA KWA WANAFUNZI SHULENI KWA ASILIMIA 100%.

Imewekwa: February 25th, 2025

Kikao cha tathimini  ya lishe ngazi ya kata kimezimia shule zote kuhakikisha zinatoa chakula  kwa asilimia 100% kwa wanafunzi  wawapo shuleni ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya ufwatiliaji wa mara kwa mara shuleni lakini pia kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Kuhakikisha kila shule imelima mazao ya chakula kwaajili ya kurahisisha upatikanaji wa Chakula Shuleni ili kuwapunguzia gharama wazazi  za kuchangia chakula .

 Anakleth  Michombero   katibu tawala  Wilaya ya Chunya akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ametoa azimio hilo leo tarehe 25/02/2025 wakati wa kikao cha Tathimini ya lishe ngazi ya kata cha robo ya pili kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Mwanginde Halmashauri ya Wilaya ya Chunya jengo jipya la utawala.

‘’Moja ya maazimio ya kikao hiki ni kuhakikisha kila shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inatoa chakula kwa asilimia 100% ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya ufwatiliaji wa karibu katika shule hizo , lakini pia niwaombe twendelee kushirikiana kkuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri katika masuala ya lishe ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi maeneo yenye mapungufu’’ amesema Michombero

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dk Zuberi Mzige ametoa rai kwa wajumbe wa kikao hicho  kwendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu pamoja na kuendelea kutoa Elimu ya kwa jamii kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa huo wa Kipindupindu na  Magonjwa maengine ikiwepo ugonjwa wa Maburg.

‘’Ugonjwa wa Kipindupindu bado ni vita katika maeneo yetu niwaombe tuendelee kuchukua tahadhari lakini pia pigeni marufuku watu kunywa maji ya kwenye mito kwasababu maji hayo yamepimwa yameonekana si salama , lakini pia Ikitokea kuna mtu  kafia nyumbani asizikwe mbaka  mbaka chanzo cha kifo kijulikane “ alisisitiza Dr Zuberi.

Vile vile Mganga Mkuu  amewataka watendaji  kufuatilia zahanati bubu pamoja na maduka ya madawa ambayo yamefunguliwa bila utaratibu katika maeneo yao  na kutoa taarifa  ili waweze kufanya ufwatiliaji na kuwawajibisha wahusika hao kwani wanatoa huduma  pasipo kufuata taratibu  na miongozo ya wizara ya afya.

Kaimu Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Simoni Mayala ameendelea kusisitiza juu ya kampeni ya serikali  ya kuhakikisha taasisi zote zinatumia nishati safi hivyo kuwataka watendaji kwendelea kujipanga kuona namna ya kutekeleza kampeni hiyo lakini pia kuhakikisha Shule zinajenga store kwaajili ya kuhifadhia chakula na majiko ya kupikia.

Aidha ameongeza kuwa kitengo cha lishe kwa  mwaka wa fedha 2026/2026  wametenga bajeti kwaajili ya mashine za kuongeza virutubishi kwenye nafaka ambapo wataanza na kata tano za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambazo ni  Makongolosi, Chokaa, Lupa ,Ifumbo, na Chalangwa  ili kwendelea kutatua changamoto za lishe .

Kikao cha Tathimini ya lishe ngazi ya kata cha robo ya pili kimehusisha idara ya Afya, elimu msingi na sekondari, Mipango na uratibu , utumishi, watendaji wa kata na waratibu wa lishe ngazi ya kata  ambapoma mbo mbalimbali  yamejadiliwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shule zinatoa chakula kwa asilimia 100%. Kwa wanafunzi wawapo shuleni.

Wajumbe wa kikao cha tathimii ya lishe ngazi ya kata robo ya pili  wakipitia na kujadili agenda mbalimbali za kikao hicho kilichoketi katika ukubi wa Mikutano wa Hamashauri ya Wilaya ya Chunya (Mwaninde hall)

Kaimu Afisa lishe Wilaya ya Chunya ndugu Simoni Mayala akielezea  mpango wa bajeti kwaajili  ya  mashine za  kuongeza virutubishi katika nafaka

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • TARAFA YA KIPEMBAWE CHUNYA YAJIDHATITI KUWATUMIKIA WANANCHI.

    March 21, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.