Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamim H Kambona amesema wilaya ya Chunya imejipanga kuhakikisha inakuwa katika Halmashauri Kumi bora katika ukusanyaji wa Mapato kitaifa kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 jambo ambalo linawezekana kwani kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 Halmashauri ya wilaya ya Chunya imevuka lengo la Makusanyo kwa Zaidi ya asilimia 140 mpaka April.
Amesema hayo Mapema leo tarehe 18/04/2024 ofisini kwake wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema Chunya inafanya vizuri katika utekelezaji wa Majukumu yake kwasababu ya Ushirikiano uliopo wakati wa utekelezaji wa Majukumu hayo.
“Tunataka kuingia kwenye 10 bora za ukusanyaji wa mapato kitafa, mbali na kwamba tumeendelea kufanya vizuri kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya lishe kwa sushika nafasi ya tatu kitaifa mara tatu mfululizo, Utoaji wa Chanjo kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa na katika utoaji wa huduma za Mpango wa Taifa wa kunusuru kaya masikini (TASAF) kwa kushika nafasi ya tatu kitaifa”. Amesema Kambona
Aidha Kambona amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na maeneo mengine kutokana na ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watumishi wote , Baraza la Madiwani pamoja na Wadau mbalimbali wa maendeleo katika Halmashauri hali iliyopelekea Chunya kwendelea kufanya vizuri katika ngazi ya kimkoa na kitaifa kwa ujumla.
“Halmashauri inafanya vizuri maeneo mbalimbali kutokana ushirikiano mkubwa uliopo kwa waumishi wa Halmashauri kwa ujumla wake, Baraza la Madiwani, Kamati ya usalama, wadau wa Maendeleo na wananchi wote kwa ujumla, na tunaendelea kuimarisha ushirikiano kwa watumishi wote bila kujali daraja la mtumishi ili kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri Zaidi”. Ameongeza Kambona
Pia Kambona amesema Halmashauri Itaendeleo kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri pamoja na kuongeza vitendea kazi kwa watumishi wote ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi ili hatimaye lengo la Serikali ya awamu ya Sita la kuwarahisishia wananchi wake upatikanaji wa huduma liendelee kutimia Chunya
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inatarajia kukusanya shilingi bilioni nane kwa mapato ya ndani mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo mwaka 2023/2024 Halmashauri itakiwa kukusanya Shilingi bilioni 5.5 lakini mpaka Aprili 5 Halmashauri imekusanya Shilingi bilioni 7.9 ambayo ni asilimia 143 ya makadirio yaliyowekwa mwaka 2023/24.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.