Mwenge wa uhuru umekamirisha ratiba yake kimkoa wilayani CHUNYA
Wilaya ya Chunya imekalimisha Majukumu makubwa mawili ndani ya siku mbili tarehe 13 na 14/09/2023 ambapo wilaya ilipokea mwenge wa uhuru na kuukimbiza Zaidi ya kilomita 260 huku miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 2.9 ikipitiwa wakati huo huo wanafunzi wa darasa la saba wamefanya mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi.
Miradi iliyopitiwa na mwenge ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Mchepuo wa Kiingereza wenye thamani ya Zaidi ya milioni 340,Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Hospitali ya wilaya ya Chunya wenye thamani ya milioni 388, ujenzi wa zahani ya Everest inayomilikiwa na vijana walionza kutekeleza mradi huo baada ya kukopeshwa fedha milioni 39 kupitia fedha zinazotengwa na Halmashauri, Mradi wa ujenzi wa maabara ya kupima sampuli za madini wenye thamani ya milioni 955,mradi wa uchimbaji visima 26 utakagharimu milioni 910, mradi wa ujenzi wa kiwanda kidogo cha kusindika alizeti na kusaga mahindi pamoja na miradi mingingine
Sambamba na miradi hiyo kupitiwa na mwenge wa uhuru wilayani Chunya Mwenge ulitoa jumbe mbalimbali maeneo mbalimbali kuhusu utunzaji wa mazingira, mapamabano dhidi ya Maralaia, mapambano dhidi ya Ukimwi, madawa ya kulevya na pia kuwasihi wananchi kuendelea kulinda, kutunza na kuhifadhi mazingira ili kuepuka ukame ambao unaweza kupelea njaa katika nchi yetu jambo ambalo sio lengo la serikali
Mwenge wa uhuru umekamilisha ratiba yake wilayani Chunya baada ya kupokelewa tarehe 13/9/2023 katika uwanja wa mpira wa miguu Sinjilili na Mkesha kufanyika katika uwanja wa mpira wa miguu Bitimanyanga na tarehe 14/9/023 Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S Mayeka alimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zaberi Homera na Baayae Mkuu wa Mkoa aliongoza msafara wa Mwenge mpaka shule ya sekondari Kiloli iliyopo halmashauri ya wilaya ya Sikonge ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Batilda Buriani aliupokea mwenge wa uhuru 2023 tayari kuukimbiza katika Mkoa wake
Mwenge wa uhuru mwaka 2023 ukiongozwa na vijana shupavu chini ya Ndugu Abdallah Shaib Kaim umekagua, umefungua na umetembelea miradi mbalimbali katika sekta ya Afya, elimu, maji na miradi ya maendeleo na mwenge wa uhuru umeridha na utekelezaji wa miradi unafanywa wilayani Chunya na umepoea miradi yote inayotekelezwa wailani Chunya
Shamlashamla za mapokezi ya mbio za mwenge wa uhuruzi uwanja wa mpira wa miguuSinjilili kata ya Itewe
Kiongozi wa mbi za mwenge ndugu Abdallah Shaibu Kaim akisalimiana na viongozi mbalimbali waserikali na chama wakati wa mapokezi ya mwenge viwanja vya Sinjilili
Mkuu wa wilaya Mh. Mayeka S. Mayeka akisoma taarifa fupi wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru uwanja wa Sinjilili
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.